fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps Google Teknolojia

Google kuleta mabadiliko ya sera kwenye programu tumishi #Android

Google kuleta mabadiliko ya sera kwenye programu tumishi #Android

Watumiaji wa simu janja za kiganjani/vifaa vya kidijiti vinavyotumia mfumo endeshi wa Android ni wengi na wanazidi kuongezeka kila siku lakini malalamiko mbalimbali yanayohusu usalama, faragha kwenye simu janja yamekuwa ni kilio cha wengi duniani kote kitu ambacho kinasabisha mabadiliko ya sera mara kwa mara.

Google lakini hata Apple wamekuwa wakifanyia maboresho ya sera zao mbalimbali kulingana na kile ambacho wateja wao wanakilalamikia ama wanaona ni vyema wakabadilisha kitu fulani ili kuweza kuvutia wateja wengi zaidi. Na katika pitapita yangu ya huku na kule nikakutana na kitu kizuri ambacho kinahusu programu tumishi zinazofanya kazi kwenye Android.

Katika mabadiliko ya sera kwenye Android haitaruhusiwa kwa programu tumishi yoyote ile kuweza kujua programu nyingine ambazo zipo kwenye rununu/kifaa husika mpaka iwe ni LAZIMA kwa kitu hicho kufanyika lengo likiwa kuweza kumsaidia mtumiaji kuweza kutumia vizuri kifaa chake.

Watengenezaji wote wa programu tumishi wanatakiwa kufanya hicho wanachokitengeneza hakina uwezo wa kuchunguza programu tumishi nyinginezo zilizopo kwenye simu janja husika vinginevyo zitaondolewa.

mabadiliko ya sera

Sababu ya Google kuamua kufanya maboresho ya sera zinazohusu programu tumishi inatokana nia ya kutoruhusu udukuzi, kutaka kuleta matangazo ya aina fulani kwa faida ya aliyetengeneza programu tumishi husika, n.k.

Mabadilko hayo ya kisera yanahusu programu tumishi za kwenye Android yanatazamiwa kuanza kutekelezwa kuanzia Mei 5 ya mwaka huu. Google wanasema watengenezaji wa programu hizo wategemee kuona vitu vyao vikiondolewa ndani ya Playstore iwapo zitakuwa hazitekelezi matakwa ya wamiliki wa duka.

Vyanzo: Gadgets 360, News Deal

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania