WhatsApp, huduma maarufu ya ujumbe-pupa imepata maboresho yaliyokuwa yakisubiriwa na wengi – muonekano mpya wa ‘Material Design’ kwenye Android. Material Design ni muongozo mpya wa muonekano wa Android na programu zake kwa mujibu wa Android, toleo la 5.0.
Muongozo huo unaleta mbadiliko ya kimuonekano kama kupanga vitu ki-gridi zaidi, kuongeza manjonjo wakati wa kufungua/ kufunga app na ‘effect’ za rangi na vivuli kwenye muonekano wa app.
Mabadiliko haya yameibadilisha sana WhatsApp kama tulivyoizoea na unaweza kujionea mwenyewe kwa mifano hii chache ya picha:
Toleo hili jipya la WhatsApp linategemewa kumfika kila mtu anayeitumia kwenye simu za Androidi kupitia Google Playstore ndani ya siku chache zijazo lakini kama unataka kuipata sasa hivi, ingia moja kwa moja kwenye kurasa yao->> hii hapa, ishushe na kupakia kwenye simi yako ya Android.
No Comment! Be the first one.