Hivi leo ukimuuliza Mtanzania anayetumia simu ya mkononi kitu ambacho kinamuumiza roho kwa walio wengi ni gharama mpya za mawasiliano (hususani vifurushi vya intaneti) ambazo zimeanza kutumia rasmi Aprili, 2 2021 kufuatia mabadiliko madogo ya kanuni kwa kampuni za simu zilizotolewa na TCRA wiki chache zilizopita.
Ikiwa ni zaidi ya saa 24 tangu makampuni ya simu zitoe gharama mpya za vifurushi mbalimbali wananchi wengi wamekuwa wakitoa kilio chao kuhusu mabadiliko hayo hasa kwenye upande wa VIFURUSHI VYA INTANETI ambavyo vinahuzunisha kwa kweli.
Kwa mujibu wa taarifa ilyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Aprili 2 ni kuwa imesitisha kwa muda gharama hizo mpya za vifurushi hususani vya intaneti kutumika mpaka watakapotangaza tena. Lakini bei mpya za vifurushi vinavyohusisha dakika za kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maneno zitaendelea kutumika kama kawaida.
Habari hii ni chereko kwa wengi na kwa saa kadhaa wale ambao kazi zetu zinategemea intaneti kwa kweli joto la jiwe tumelipata. Tunaomba makampuni ya simu iturudishe kule tulipokuwa awali.
Tupe maoni yako ewe msomaji wetu wetu kufuatiatia taarifa hii kutoka kwenye mamlaka husika. Usiache kutufuatilia kila leo kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia ndani na nje ya Tanzania.
Vyanzo: Gazeti la Mwananchi, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.