fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android apps Teknolojia

Android N, toleo lijalo la Android – Fungua na tazama apps mbalimbali kwa wakati mmoja

Android N, toleo lijalo la Android – Fungua na tazama apps mbalimbali kwa wakati mmoja

Spread the love

Uwezo wa kufungua na kutumia apps nyingi kwa wakati mmoja mithili ya kwenye kompyuta unakuja kwenye Android, na unategemewa kuwepo ndani ya toleo lijalo la Android linalofahamika kwa sasa kwa jina la Android N.

Watu wanaotumia toleo hilo la Android lililokwenye matengenezo wameona uwepo wa uwezo huo wiki hii, na waliojaribisha wamesema uwezo huo unafanya kazi vizuri tuu.

SOMA PIA  Google Inaweza Ikabadilisha Muonekano Wake Katika Simu Janja!

android N uwezo Fungua na tazama apps mbalimbali

Kama uwezo huu utawezeshwa na kutumiwa ipasavyo basi watumiaji wa simu au tableti zenye vioo(display) kubwa watufaika zaidi na uwepo wa teknolojia hii.

Na kwa Google suala hili litafanya tableti zake zipendwe zaidi kwani itarahisisha zaidi utumiaji wa apps nyingi kwa wakati mmoja – jambo ambalo kwa wakati mrefu limeshindikana kwenye tableti za Android na iOS. Ni tableti zinazotumia toleo la Windows kutoka Microsoft ndio zenye uwezo huo.

SOMA PIA  Kuwa sehemu salama dhidi ya wadukuzi

 

Fungua na tazama apps mbalimbali

Endelea kutembelea chanzo chako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia – TeknoKona!

Vyanzo: AndroidPolice na ArsTechnica 

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania