fbpx
apps, Teknolojia

Programu tumishi inayoweza kutambua kuzidi kiwango cha dawa yaundwa

programu-tumishi-inayoweza-kutambua-kuzidi-kiwango-cha-dawa-yaundwa
Sambaza

Inaweza kupita muda mrefu hujakumbwa na ugonwa wowote lakini inafahamika kabisa unapoumwa inakubidi utafute tiba ili uweze kupona. Vilevile, suala zima la kuzidishiwa kiwango cha dawa ni jambo ambalo lipo na linawezekana.

Unapokwenda kutafuta tiba kwenye kituo cha afya, zahanati au hospitali vifaa vinavyotumika kumpima mgonjwa ili kuweza kujua anasumbuliwa na nini vimetengenezwa kuendana na dunia ya leo ambayo iliyotawaliwa na sayansi bila kusahau teknolojia.

Sasa wanasayansi/watafiti kutoka Chuo Kiuu cha Washington, Marekani wametengeneza programu tumishi waliyoiita Second Chance (nafasi ya pili) ambayo inaweza ikatambua iwapo umezidisha kiwango cha dawa na kisha kuweza kutoa taarifa kwa ajili ya msaada zaidi.

Watafiti hao wamekuwa wakipata msukumo wa kutengeneza programu hiyo kutokana na watu takribani 110 kufa kila siku kutokana na kujizidishia madawa ambayo mengine hayaruhusuwi kabisa mathalani madawa ya kulevya.

kiwango cha dawa
Programu tumishi inayoweza kuytambua iwapo kiwango cha dawa kimezidi yaundwa hata katika umbali wa futi tatu.

Inafanyaje kazi?

Programu hiyo inafuatilia namna ambavyo mtu anapumua kwani mtu ambae amezidisha kiwango cha tiba (dawa) namna anavyopumua hubadilika kabisa hivyo kitu ambacho programu tumishi inafanya ni kutuma mawimbi ya sauti kimya kimya kwenye kifua cha mlengwa kisha itafuatilia namna ambavyo mhusika anapumua na kama atakuwa amezidisha tu itapiga simu kwa rafiki/ndugu au huduma ya dharura ili kuja kutoa msaada zaidi.

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kujizuia Na Uraibu (Addiction) Wa Kutumia Simu Janja Kila Mara!
kiwango cha dawa
Kama mhusika atashindwa kutoa ushirikiano basi programu hiyo itampigia mtu ili kuja kutoa msaada.

Ipo katika hatua ya majaribio.

Programu husika iwekwa kwenye Samsung Galaxy S4 na kuweza kuwa sahihi kwa 96%; wahusika waliacha kupumua kwa karibu sekunde 10 au chini ya hapo kama kiashiria cha kuzidisha dawa, 87% ya kesi katika majaribio ilionyesha ni kweli viwango vyao vya upumuaji vulipungua. Pia, iliweza kuhisi matukio 19/20 yanayoashiria kuzidishwa kwa dawa.

Bado programu hiyo haijaletwa kwa wengi kwani haijaidhishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa, Marekani na ikisharuhusiwa basi italetwa kwa watu kwa ajili ya matumizi. Je, unaizungumziaje programu husika?

Vyanzo: The Verge, Scientific American

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|