fbpx
apps, instagram, Teknolojia

App ya kujitegemea ya Instagram Direct kuondolewa!

instagram-direct-kuondolewa-hivi-karibuni
Sambaza

Instagram Direct imekuwa ikiambatanishwa kwenye app ya Instagram lakini pia kumekuwa na mjaribio ya kuigeuza kuwa app ya kujitegemea. Tayari Facebook waliingiza app ya kujitegemea kwenye takribani nchi 6.

Facebook wamekuwa ni watu wa kutoa masasisho kila mara na yamekuwa yakijumuisha maboresho makubwa kwa madogo. Kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya majaribio ya kuwa na app inayojitegemea ikienda kwa jina la Instagram Direct na ikiwe imelenga kuwa mshindani wa moja kwa moja wa Snapchat.

INAYOHUSIANA  Uundaji wa iPhone 12 unaendelea kama kawaida
app ya Instagram Direct
Angalizo lililotolewa kwa watumiaji wa app ya Instagram Direct

Katika taarifa za hivi karibuni zinaonesha kuwa Facebook wanaachana na mpango huo.

Je, Instagram Direct ni nini?

Hiki ni ile alama ya tiara au jumlisha (+) inayoonekana upande wa klia juu baada ya kuingia kwenye Instagram. Kazi yake ni kuwezesha kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa maandishi katika faragha au kama vijana wanavyosema “Nifuate DM” 😆 😆 .

Instagram Direct
Ukurasa unamuwezesha mtumiaji wa instagram kutuma/kusoma jumbe alizopokea kutoa kwa watu waliojiunga huko.

Je, hatua hiyo ina maana haitawezekana tena kutuma/kupokea jumbe kwenye Instagram?

La hasha! Watumiaji wa Instagram wataendelea kutuma na kupokea jumbe kama kawaida. Facebook itakuwa imeona katika masoko waliofanyia majaribio huduma hiyo kujitegemea haijapokelewa vizuri na hivyo wameamua kuachana na mpango huo.

INAYOHUSIANA  Youtube: Kipengele cha Dark Mode kwenye simu

Vyanzo: Phone Arena, TechCrunch

{Makala hii ilikuwa na makosa na imefanyiwa maboresho 20/05/2019)

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|