Imesemekana kwamba Korea kaskazini imefanya jaribio lililofanikiwa la injini ya roketi kwaajiri ya makombora ya masafa marefu, kama habari hizi ni za kweli basi nchi hiyo sasa imepata uwezo wa kushambulia ardhi ya marekani na maadui wake wengine kutokea Korea .
Afisa mmoja wa jeshi la Korea kusini amesema kwamba wamegundua kupitia shirika la habari la Korea Kaskazini kwamba nchi hiyo imefanya jaribio la injini ya roketi kwa ajiri ya makombora ya masafa marefu na kwamba wanaendelea kufuatilia nyendo za nchi hiyo iwapo watapanga kufanya shambulizi.
Kwa maneno mepesi ni kwamba Korea Kaskazini tayari wamedai wanayo mabomu ya nyukilia na wamekuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakitamba kwamba watayatumia iwapo watachokozwa, lakini nchi hiyo haikuwa na uwezo wa kuipiga Marekani kwa kutokea katika nchi yao hivyo teknolojia hii itawaruhusu kusafirisha mabomu katika roketi ambayo itaruka kutoka nchini mwao mpaka Marekani.
Teknolojia hii ni hatari sana kwa amani ya dunia maana kwa hari ilivyo sasa iwapo tu Raisi wa nchi hiyo ataamua kuipiga nchi yeyote kwa kombora lake hilo basi upo uwezekano mkubwa akafanikiwa.
Ikumbukwe kwamba mwaka 1962 ulitokea mgogoro katika ya Marekani na iliyokuwa USSR wakati huo hii ilitokea baada ya Marekani kugundua uwepo wa siraha za kivita nchini Cuba, USSR kama ingekuwa na teknolojia ambayo Korea Kaskazini wanayo leo basi historia ingekuwa tofauti maana USSR walipeleka mabomu yao Cuba ili tu waweze kuipiga marekani maana wasingeweza kuipiga kutokea Kiev.
Marekani kwa upande wake ina washirika wengi Ulaya na pia Asia hivyo kuishambulia korea ya kaskazini sio swala gumu saana kwani wanaweza kuipiga kutokea katika nchi yeyote washirika.
Korea Kaskazini imefanya jaribio hili kuwaonesha mahasimu wake kwamba haifanyi mzaha juu ya matamshi yake juu ya uwezo wa kupiga ardhi ya marekani. Jaribio hili limefanywa wakati ambapo Mahasimu wa korea kaskazini yaani Marekani ikishirikiana na Korea Kusini wakiwa katika mazoezi ya pamoja ya kivita.