fbpx
HP, Kompyuta, Teknolojia

HP na kompyuta kwa ajili ya wanafunzi

hp-na-kompyuta-kwa-ajili-ya-wanafunzi
Sambaza

Telnolojia bila kuwa umeelimika daima utakuwa unaona kuwa kuna kitu umepungukuiwa ili kuweza kufurahia ulimwengu wa kidijiti na pale utakafanya maamuzi ya kuitafuta elimu basi kuwa na kompyuta kwa ajili ya wanafunzi litakuwa suala la kawaida sana.

Ngamizi maarufu kama kompyuta lakini ukitaka kuzungumzia zile zinazobebeka kirahisi tunasema “Vipakatalishi” ambavyo vipo katika makundi mbalimbali mathalani zenye uwezo wa kawaida, kati na mkubwa zaidi.

Siku si nyingi zilizopita HP walizindua kompyuta mpakato mbili ambazo wameziunda kwa kulenga watu ambao wanasoma kwa lugha nyingine ni wanafunzi. Sasa kwanini ngamizi hizo zinawafaa zaidi wanafunzi? Kupata majibu tazama jedwali lifuatalo:-

INAYOHUSIANA  Bibi wa miaka 81 atengeneza app yake ya kwanza kwa ajili ya iOS

Kipengele

HP Chromebook x360 11 G2

HP Chromebook 11 G7 EE

Kioo Kioo kina urefu wa inchi 11  (1366 x 768px) IPS ambacho pia ni cha mguso Kioo kina urefu wa inchi 11 lakini sio cha mguso katika matoleo mawili tofauti; IPS na SVA
Muonekamo Ina uwezo wa kuzungushwa mpaka nyuzi 360 na kuitumia kama tabiti Inaweza kuzungushwa mpka nyuzi 180 pekee (haiwezi kutumika kama tabiti)
Kipuri mama Dual-core Celeron N4000 ama  quad-core N4100 Dual-core Celeron N4000 ama  quad-core N4100
kwa ajili ya wanafunzi
Hii ndio HP Chromebook x360 11 G2

Kipengele

HP Chromebook x360 11 G2

HP Chromebook 11 G7 EE

RAM/Diski uhifadhi
 • 8GB RAM kwa GB 32/64 memori ya ndani.
 • 8GB RAM kwa GB 32/64 memori ya ndani.
Betri

Inakaa na chaji kwa muda wa saa 11.5

Inakaa na chaji kwa muda wa saa 13

Mengineyo
 • Inatumia kalamu janja
 • Uzito: Kg 1.47
 • Ina sehemu mbili za USB Type C,
 • Sehemu moja ya USB Type A
 • Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni (mm 3.5)
 • Ina sehemu  ya kuweka memori ya ziada
 • Uzito: Kg 1.47
 • Ina sehemu mbili za USB Type C
 • Sehemu moja ya USB Type A
 • Sehemu ya kuchomeka spika za masikioni (mm 3.5)
 • Ina sehemu  ya kuweka memori ya ziada
kwa ajili ya wanafunzi
Muonekano wa HP Chromebook 11 G7 EE.

Bei zake zinatarajiwa kufahamika hapo baadae lakini zitaingia sokoni mwezi Aprili 2019. Vipi vipakatalishi hivi umependezwa navyo?

Vyanzo: GSMArena, Androi Police

INAYOHUSIANA  Simu Nyembamba Zaidi Kutengenezwa Siku Zijazo

 

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|