fbpx
Teknolojia

Teknolojia 7 Zilizotisha Kombe la Dunia 2014


Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Kombe La Dunia Brazil 2014

Kombe la dunia la mwaka huu limekuwa la kuvutia kutokana na maoni ya watu wengi. Kombe hilo limepambwa na rekodi kadhaa za kufurahisha ikiwemo magoli mengi zaidi yaliyowahi kufungwa kwa michuano hiyo. Sifa nyingine kubwa ni kuwa michuano ya aina yake yaliyopambwa kwa matumizi makubwa na ya watu wengi kiteknloljia yaliyowahi kuonekana au kusikika. Hizi ni teknolojia saba zitakozokukumbusha jinsi maisha ya mwanadamu na soka yalivyobadilika:

 

Namba 1: Teknolojia ya golini99.889.982
Wadau wengi watakumbuka England na Ujerumani Kombe la Dunia 2010, Afrika ya Kusini ambapo Wajerumani waliwaengua Uingereza kwenye kinyang’aniyro kwa magoli 4-1 huku Uingereza wakilalamika kunyimwa goli halali. Watu wengi wanasema kama goli lile lingeruhusiwa, lingebadilisha kabisa sura ya mechi hiyo, hata kupelekea kwa ushindi wa Waingereza.

Goli la Uingereza Vs. Ujerumani, 2010

Tangu kipindi hicho shirikisho la Dunia, FIFA limekuwa likishawishiwa kuingiza teknolojia ya golini kwenye michuano yake. Mwaka huu, dunia imeshuhudia teknolojia hiyo ikitumika kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la dunia na Juni 15, 2014, goli la pili la Ufaransa dhidi ya Honduras lilikuwa mara ya kwanza teknolojia hii kutumika kutambua goli kwenye michuano hiyo. Teknolojia hii inakuja katika fleva kadhaa. Nyingi hutumia kamera zenye kasi sana na nyingine hutumia sumaku Ili kutambua goli. Inachukua sekunde chache tu kwa taarifa za goli kufika kwa refa kutumia teknolojia ya mionzi iliyokuwa na ulinzi maradufu wa kuzuia ‘mahacker’ kuleta uharibifu wao.

INAYOHUSIANA  Pakistan Yapiga Marufuku BlackBerry Enterprise Services (BES) Kutokana Na Sababu Za Kiusalama!

teknolojia ya golini

 

 

Namba 2. Povu Linalopotea:

Povu hilo linalojulikana kama “Vanishing foam” kwa lugha ya kigeni linatengenezwa kwa asilimia kubwa na maji na gesi ya butane pamoja na vitu vingine. Teknolojia hii imeweza kutumiwa kwa mara ya kwanza kwenye kombe la dunia mwaka huu. Marefa wanatumia hii kuhakikisha wazuiaji wa mipira ya adhabu wanabaki mita 9.7 mbali na mpira. Povu lake linapotea baada ya dakika moja baada ya kupulizwa. Ingawa imetumika sana, wadau wengi wameonyesha kutoridhika na teknolojia hiyo wakisema bado haijaweza kuzuia wakabaji kujongea karibu na mpira pale unapopigwa. Teknolojia hii ilionekana mara ya kwanza Uingereza, miaka ya 1980 ikiwa inapendekezwa na kampuni iliyoundwa na kiungo maarufu wa Manchester United, Sir Bobby Charlton ingawa shirikisho la soka la Unigereza halikuvutiwa nayo.

 

Namba 3: Simu-janja na mitandao ya kijamii.
Tukio la kombe la dunia la mwaka huu limevunja rekodi ya mazungumzo kwenye mitandao ya jamii. Hii ni kwa Subabu ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa kwenye teknolojia ya mawasiliano, hususani kwenye simu za mikononi. Ripoti zinaonyesha mitandao ya Twitter na facebook ndio inayoongoza kwa mada za kombe la dunia. Twitter imeweza kuwaingiza watumiajia wake kwenye mandhari ya kikombe la Dunia zaidi kuweza kuwashirikisha na kuwaletea habari karibu zaidi. Wakati Brazil ilipowafunga Chile kwa penati, tweet million 16.4 zilitumwa duniani kote na kufanya kuwa tukio liliozungumziwa na watu wengi zaidi duniani katika mtandao huo. Tukio hilo Ilivunja rekodi ya mazungumzio ya uchaguzi wa uraisi wa marekani mwaka 2012. Mtandao wa facebook pia umeripoti kuwa kufikia Juni 30, iliweza kupata gumzo la harakati zaidi ya billioni moja la tukio hilo la dunia.

INAYOHUSIANA  Je kwa nini diski zinaanza na namba C badala ya A? #Windows

 

Namba 4: Mpira wa Brazuca!Fifa-world-cup-2014-brazil-Stadium-wallpaper1
Addidas waja na mpira mpya kwa kombe hili la dunia unaoitwa Brazuca. Mpira huu umesifiwa zaidi na wachezaji na makocha wa timu za mataifa. Neno ‘Brazuca’ inatokana na maoni ya watu wengi kwenye mtandao. Neno hilo ni neno la mtaani la Brazil linalomaanisha hali ya ubrazilli na raha ya kuishi kibrazili. Brazuca una mabadiliko mengi yakiteknolojia unaobadilisha jinsi utavyoweza kupaa angani. Mpira huu umejaribiwa sana katika kipindi cha miaka miwili na nusu kuwepa makosa yaliyofanywa na Addidas kwenye kombe la dunia lililopita kwa mpira wa Jabulani. Mpira huo uliowachukiza wachezaji wengi ikiwamo makipa Iker Cassilas wa Hispania na Gianlugi Buffon wa Italia.

 

Namba 5: Jezi na viatu mbalimbaliWARRIOR_SKREAMER__BLUE_GREEN_WEB-HEADER_909x376
Nike, Addidas na Skreamer pamoja na watengenezaji wengine wa jezi na viatu vya mpira wameweza kupamba kombe la dunia na teknolojia inayowezesha wachezaji kufanya mambo yao uwanjani kwa makini. Vifaa hivyo ni kama Nike Mecurical, kiatu chenye uzito wa gramu 190 kinachovaliwa na wachezaji Christiano Ronaldo, Ribery, Edin Hazzard amabacho ni chepesi na chenye kimwezesha mchezaji kukimbia kwa spidi na Screamer ‘Warrior’ kiatu ambacho kimevaliwa na wechezaji ikiwemo beki wa ubelgiji Vincent Kompany.

INAYOHUSIANA  Uwekezaji katika sarafu ya za kidijitali nchini Tanzania

 

Namba 6: Teknolojia Kufuatilia Wachezaji
Wachambuzi wa soka hupenda kuzungimzia uwezo binafsi wa wachezaji kama kasi na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufunga magoli. Timu kama Colombia na Marekani zimetumia teknolojia tofauti za SportVU na Catapult kuwasaidia kusoma mienedo ya wachezaji wao mazoezini na uwanjani ili kupata ‘data’ za ufanisi wa harakati zao. Makocha hutumia data hizi kurekebisha makosa ya wachezaji na kuwaongoza kutumia uwezo wao.

 

Namba 7: Suti ya Kiroboti

anigif_enhanced-24067-1402601516-1
Suti hiyo ilitumika Juliano Pinto, mtu aliyepoteza uwezo wa kutembea kupiga mpira na kufungua kombe la dunia. Pinto aliweza kufanya hivyo kufikiria tendo analotaka kufanya, yani kupiga mpira na kompyuta kwenye roboti hiyo iliweza kuchukua wazo hilo na kueleza suti kupiga mpira kufungua kombe la dunia. Watu wengi nchini Brazil na kote duniani wanaongelea teknolojia hiyo mpya ambayo itaweza kubadilisha dunia kwa watu walemavu kuweza kufanya vitu ambavyo walifikiria havitaweza kufanywa na wao. Teknolojia hii bado ni changa ila kuna matumaini makubwa.
Hakika, kombe hili limeweza kuwa kombe litakumbukwa kwa teknolojia kutumika kwa wingi na kwa njia ya kipekee kuonyesha jinsi dunia ya binadamu ilivyobadilika kuanzia matumizi uwanjani hadi kwa mashabiki.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*