fbpx
Kompyuta, Microsoft, Windows, Windows 10

Windows 10 kula nafasi kubwa zaidi ya diski, kupakua masasisho yenyewe

windows-10-kula-nafasi-kubwa-zaidi-ya-diski

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Habari mbaya kwa watumiaji wa Windows wanaotumia diski zenye ukubwa mdogo, Windows 10 kula nafasi kubwa zaidi muda si mrefu.

Tayari watumiaji wengi wa Windows 10 wanalalamika ujio wa masasisho (updates) mbalimbali za Windows ambazo muda mwingine ndio uharibu mambo.

Microsost wamesema wanaongeza kitu kinaitwa ‘Reserved Storage’ katika toleo la Windows 10 – Build 1903. Reserved Storage, yaani Nafasi Iliyohifadhiwa itakuwa na ukubwa wa hadi GB 7 na itatumika tuu kuhifadhi matoleo ya masasisho ya Windows 10 yatakayoshushwa (download) moja kwa moja na Microsoft kutoka kwenye mtandao na kuhifadhiwa kwenye nafasi hii kabla ya mtumiaji kupewa taarifa ya kuweza kupakua/kuinstall kwenye kompyuta.

INAYOHUSIANA  Toleo la Kivinjari cha Microsoft Edge chenye misingi ya Chromium lavuja
Windows 10 kula nafasi kubwa
Windows 10 kula nafasi kubwa zaidi ya diski: Hivi karibuni masasisho mapya (updates) ya Windows 10 mengi yamekuwa yanakuja na matatizo mbalimbali

Microsoft wamesama kwa sasa teknolojia hiyo inakuja kwenye laptop mpya zitakazokuja na Windows 10 toleo la 1903 ila muda si mrefu itasambazwa kwa hata watu wanaotumia kompyuta/vipakatalishi za miaka ya nyuma. Kwa sasa kuna toleo 1809.

Suala hili hili linaleta changamoto kwa watumiaji wa aina mbili wa Windows kwa sasa;

  • Wale wenye nafasi ndogo za diski, kwani GB 7 ni kiasi kikubwa sana kama diski ya kompyuta husika tayari ina vitu vingi.
  • Wale wasiopenda sasisho kujidownload bila ruhusa, wengine hawapendi tuu kuhamia matoleo mapya mapema na wengine wana wasiwasi na data zao.
INAYOHUSIANA  Vitu Kwenye Windows Ambavyo Microsoft Hawawezi Kuvijibu!

Vipi je, wewe ni mtumiaji wa Windows 10, una mtazamo gani na uamuzi huu wa Microsoft?

Chanzo: Forbes na tovuti mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |