fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Facebook Mtandao wa Kijamii

Facebook warahisisha jinsi ya ku-add marafiki Messenger

Facebook warahisisha jinsi ya ku-add marafiki Messenger

Spread the love

Messenger app ya Facebook kwa ajiri ya kuchati ipo mbioni kuleta njia tatu mpya kwaajiri ya kuweza ku-add marafiki katika app hiyo, huu ni ushahidi kwamba Messenger inajaribu kupambana na Snapchat na mitandao mingine kupata watumiaji wapya.

Mtandao huu unajaribu kuwa mtandao rafiki kwa watumiaji kwa maana jinsi mtandao unavyokuwa ni rahisi kutumia ndivyo ambavyo mtandao unavyoweza kupata wateja wengi na kuwa maarufu.

ku-add

Watumiaji wakionesha utumiaji wa code kwaajiri ya ku-add marafiki

Messenger imeleta namna zifuatazo mpya za kuweza ku-add marafiki katika mtandao huu kama ifuatavyo

  • Kuadd marafiki kwa kutumia username.

Hii ni njia ambapo mtumiaji anaweza kumuongeza rafiki katika orodha ya marafiki wake kwa kuandika jina ambalo mtumiaji analitumia katika Messenger. Njia hii sio ngeni kwani ndiyo inatumiwa na mitandao mingine ya kijamii kama vile Twitter.

  • Ku-add marafiki kwa kutumia link.

Njia hii itawapatia watumiaji link ambayo unaweza kuwapatia marafiki zako kwa njia yeyote ile na pindi watakapo bofya linki hiyo watapelekwa moja kwa moja katika ukurasa wako wa Messenger.

  • Ku-add marafiki kwa kutumia Code.

Hii ni njia mpya ambayo tumeanza kuiona sana katika mtandao wa Snapchat, njia hii inamtengenezea code mtumiajia ambapo ili kumuadd rafiki yako unatakiwa kui scan code hiyo ambayo itakupeleka moja kwa moja katika ukurasa wa rafiki yako.

SOMA PIA  TikTok yaongeza vipengele vya mapato kwa watengeneza maudhui, ikijumuisha vidokezo na zawadi za video

Yote kwa yote hizi ni jitihada za Messenger kuweza kubaki katika chati hasa katika kitengo hichi cha mitandao ya kijamii ambacho kwa siku za karibuni kimekuwa na ushindani mkubwa sana.

Comment

Comments

  1. […] post Facebook warahisisha jinsi ya ku-add marafiki Messenger appeared first on […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania