Mtandao wa kijamii wa X, uliokuwa ukifahamika kama Twitter, unategemea kuja na uwezo wa kupiga simu za video na sauti kwa watumiaji wake. Elon Musk, mmiliki wa mtandao wa X, alitoa taarifa kupitia andiko lake kwenye mtandao huo wa kijamii.
Vipengele vipya vitakuwa available kwenye iOS, Android, Mac, na PC, na havitahitaji nambari ya simu. Elon Musk analengo la kuifanya app ya mtandao huo kuwa na uwezo wa kufanya mambo mbalimbali kwenye teknolojia za mawasiliano na masuala ya kifedha. Soma zaidi -> Twitter kuwa X, Elon Musk anasema mtandao huo utakuwa ‘a super App’
Kuongezwa kwa vipengele vya simu za sauti na video kwa X ni hatua kubwa itakayowafanya watumiaji wake kuwasiliana kwa urahisi bila ulazima wa kupeana namba za simu.
Haijulikani ni lini haswa vipengele vya simu za sauti na video vitazinduliwa kwa watumiaji wa X. Hata hivyo, Musk amesema kuwa “vinakuja hivi karibuni.”
Kuongezwa kwa vipengele vya simu za sauti na video kwa X ni ishara ya dhamira ya Musk kwa jukwaa hilo. Amesema anataka X kuwa jukwaa la “metaverse”, ambapo watumiaji wanaweza kuwasiliana na kushirikiana na kila mmoja katika ulimwengu wa mtandaoni/kigigitali.
Tutaendela kusubiri na kuona jinsi vipengele vya simu za sauti na video vitakavyokuja kwenye app hii na jinsi vitakavyopokelewa na watumiaji wa X. Hata hivyo, ni nyongeza muhimu kwa jukwaa hilo, na huenda vikasaidia kuifanya X kuwa na ushindani zaidi na majukwaa mengine ya kijamii kama WhatsApp.
No Comment! Be the first one.