fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtandao wa Kijamii Twitter

Twitter Kuja Na Kipengele Cha ‘Unmention’, Tukifahamu Kidogo!

Twitter Kuja Na Kipengele Cha ‘Unmention’, Tukifahamu Kidogo!

Spread the love

Twitter mara kwa mara imekua ikifanya maboresho na kuongeza vipengele vingi katika mtandao wake, hii ikiwa na dhima bora ya kuboresha huduma yake.

Mfanyakazi kutoka kitengo cha faragha anejulikana kwa jina Dominic Camozzi, ameweka wazi katika moja ya post zake kuwa hivi karibuni mtandao utaweza kukuruhusu kujitoa katika mazungumzo.

Twitter App

Twitter App

Ni kawaida sana kwa Twitter kujishangaa bado upo ndani ya mazungumzo ya watu hata kama umeshamaliza kutoa yako ya moyoni au hutaki tena kuwepo tu!.

Sasa utawezaje kujitoa katika mazungumzo hayo? kumbuka huduma hii kwa kiasi kikubwa ipo katika mazungumzo ya inbox tena yale ya kikundi ndio mtu unaweza kujitoa.

SOMA PIA  FAHAMU 'Twitter Blue' Ni Nini!

Ili kufanikisha hili kama kipengele hichi kikitoka basi huna budi kuchagua “Unmention yourself from this conversation”  ili kuweza kuachana na mazungumzo hayo mara moja

Kingine ni kwamba kipengele hichi bado hakijaweka wazi kwamba kitaanza kupatikana kwa kila mtu au kitakua kinapatikana kwa watumiaji wa Twitter Blue tuu.

SOMA PIA  Snapchat yaleta Emoji zinazotembea na video

Soma Kuhusu Twitter Blue  —–> Hapa <—–

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment, usisite kuaniambia hili unalipokeaje!

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania