Makampuni ya teknolojia mengi yanapitia magumu na mengi kimbilio lao kubwa limekua ni kupunguza baadhi ya wafanya kazi katika makampuni yao.
Meta, kampuni ambayo inamiliki mitandao ya Facebook, WhatsApp Na Instagram imeweka wazi mpango wake wa kupunguza maelfu ya wafanyakazi.
Namba halisi ya wafanya kazi ambayo itapunguzwa haijawekwa wazi lakini idadi ya watu zaidi ya 87,000 waliripotiwa mwezi September kuwa wanafanyakazi Meta.
87,000 hawa wanatoka kwa mitandao mbalimbali na makampuni mengine ambayo yanamilikiwa na kampuni ya Meta. Kupunguzwa kwa maelefu ya kazi ni wazi kuwa jambo hili sio zuri kabisa maana watu watakosa ugali wao kupitia kampuni hiyo.
Mtandao wa Wall Street Journal (WSJ) umeripoti kuwa upunguzaji wa wafanyakazi hao unaweza ukawa ni mkubwa sana hata ukilinganisha na ule wa twitter –7,500 – kwa upande wa nguvu kazi.
Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni kubwa la kiteknolojia kama Facebook kua na mpango wa kupunguza au kupunguza wafanyakazi.
Facebook mwezi September waliacha kuajiri watu wapya –milango ilifungwa kabisa—na hichi kilikua ni moja ya kiashiria kwamba siku za mbeleni wangeweza hata punguza wafanyakazi ambao wako katika kampuni hiyo.
Zuckerberg ambae ni mmiliki wa Meta hapo nyuma alisema kuwa kampuni kwa mwaka 2023 ina malengo mengi miongoni ikiwa ni:
- Uwekezaji mkubwa katika maeneo machache ya muhimu
Ili kuwezesha hili ni wazi kabisa kuna baadhi ya timu zitakua, zingine zitapungua au hata wengine kupunguzwa kazi kabisa.
Facebook kwa sasa inasema kuwa ina watumiaji wengi wa mwezi –ambao wanatumia mara kwa mara – mtandao huo na ni moja kati ya mitandao mikubwa kabisa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hili umelipokeaje? Unadhani ni sawa kwa kampuni kufanya hivi ili kuendana na mipango yake?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.