Masaa machache baadae kampuni ya Facebook inc inategemea kuzindua rasmi mtazamo mpya wa mtandao wa jamii maarufu duniani wa Facebook. Hii itafanyika makao makuu yake yaliyopo jijini California huko Marekani.
Mabadiliko hayo yanategemewa hasa kutokea kwenye ‘News Feed’, ‘News Feed’ ni ukurasa wa kwanza wa Facebook unaokutana nao ukisaini kuingia mtandaoni. Ukurasa huu huwa unakupatia habari mbalimbali kutoka kwa marafiki zako, hii ikiwa na ‘status’, na mambo mengine yahusiyo rafiki zako.
Facebook Inc hajatoa habari zaidi juu ya mabadiliko yatakayokuwepo, tutawaletea habari zaidi ya vitu vipya hapo itakapooneshwa rasmi!
No Comment! Be the first one.