Kama wewe ni mtu unayechukia kuchaji simu kila siku au kwa wale wenye ndugu au wenyewe wanaishi kwenye mazingira ambayo suala la umeme ni la shida kidogo basi Nokia 105 ndiyo simu ya kuitafuta kwa sasa.
Nokia 105 inategemea kuingizwa sokoni kipindi chochote kwa sasa na itauzwa dola za marekani 20, hivyo nategemea itauzwa takribani shillingi 30,000/= za Kitanzania.
Kwa bei hiyo unapata simu yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa siku 35 kwenye ‘standby’-ikiwa na maana kwa matumizi mengi inaweza ikashuka kidogo. Pia ina redio ya FM, pamoja na uwezo wa kuweka kengere za kumbukumbu (alarm), na inakuja na kioo cha rangi.
No Comment! Be the first one.