Baada ya kuwa na mwaka mbovu kimapato kampuni ya HTC imeibuka na simu ya kipekee.
Kampuni ya HTC ni kampuni inayokubalika sana kwa upande wa ubunifu lakini imekuwa inajikuta bidhaa zake hazifanyi vizuri sokoni kulinganisha na bidhaa za Apple na Samsung. Tofauti kubwa imeonekana HTC hawajawa wakiweka fungu kubwa la pesa katika kuzitangaza bidhaa zake kama washindani wake wafanyavyo, hivyo kufanikiwa kwa HTC ONE kutategemea sana jinsi gani kwa wakati huu watajikita katika kuitangaza.
Ubunifu wa HTC ONE (M7) ni wa hali ya juu na uwezo wake ni mkubwa sana kulinganisha na simu zingine zote zilizopo sokoni kwa sasa.
Baadhi ya uwezo wa kipekee ni pamoja na kuwa na spika mbili za stereo pamoja na amplifaya na hivyo kutoa sauti yenye kiwango cha juu. Pia kwa wale wenye ‘Smart TVs’ basi ukiwa na HTC ONE huitaji kubeba rimoti kila saa, HTC ONE inaweza kutumika kama rimoti. Kingine zaidi ni kamera yenye uwezo mkubwa sana, utakapo’click’ basi kamera hiyo itapiga picha 20 na video ya sekunde 3 kwa mara moja-vyote vitafanyika kwa wakati mmoja ndani ya sekunde 3.
HTC ONE inatumia programu ya uendeshaji ya Android 4.1 (Jelly Bean).
- Kioo cha inchi 4.7 HD (1920 x 1080 pixels)
- Prosesa -Quad core Qualcomm Snapdragon, 1.7GHz
- RAM 2GB
- Ukubwa Uhifadhi wa GB 32 au 64
- Bluetooth 4.0
- WiFi, DLNA, 4G LTE, DLNA
- microUSB port na 3.5mm audio jack
No Comment! Be the first one.