fbpx

Gemu, simu, Uchambuzi, Xiaomi

Black Shark 2 Pro – Simu janja ya GB 12 za RAM kwa wapenda magemu

black-shark-2-pro-simu-janja-magemu

Sambaza

Simu zinazotengenezwa spesheli kwa ajili ya wanaopenda kutumia simu zao kwa ajili ya uchezaji wa magemu zimeanza kuwa maarufu. Leo ifahamu simu ya Black Shark 2 Pro ambayo imetambulishwa siku chache zilizopita nchini Uchina.

Soko la simu janja zinazotengenezwa spesheli zikiwafikilia wacheza magemu limezidi kukua. Makampuni kama Asus, Razer, ZTE wameshaleta simu spesheli kwa ajili ya wacheza magemu.

BlackShark 2 Pro

Simu ya Black Shark 2 Pro ni toleo la pili la simu ya familia ya Black Shark zinazotengenezwa na kampuni ya Xiaomi. Toleo la kwanza la simu ya Black Shark 2 lilitolewa mapema mwaka huu.

 

Sifa na uwezo wa simu

Black Shark 2 Pro
Black Shark 2 Pro
  • Kwa kuwa magemu yanachezwa kwa kasi display/kioo kina teknolojia ya kuhisi mguso kwa kasi sana ambapo ni kwa kipimo cha mili-sekunde 34.7
  • Pia ni simu ya pili kuja na prosesa ya kisasa zaidi kutoka Qualcomm, hii ikiwa ni prosesa ya Snapdragon 855 Plus. Simu nyingine inayokuja na prosesa hiyo ni simu janja ya kuchezea magemu kutoka kwa kampuni ya Asus.
  • Pia simu inakuja na teknolojia ya kupooza joto kwa mfumo wa vimimina (Liquid cooling system), hivyo utaweza kucheza magemu kwa muda mrefu bila simu kupata joto sana
  • Display yake ya inchi 6.39 (2340×1080) ni ya teknolojia ya AMOLED, display imekuja na teknolojia spesheli inayowezesha sehemu flani wakati wa kucheza gemu kuweze kuleta matokeo tofauti pakuguswa (Magic Touch)- kutategemeana kama utagusa kwa nguvu sana au kidogo tuu. Hii itasaidia kurahisisha uchezaji wa magemu.
  • Kuna matoleo mawili ya Black Shark 2 Pro, yote yakija na RAM ya GB 12 ila tofauti ikiwa ni kwenye diski uhifadhi ambapo kuna toleo la GB 128 na lile la GB 256.
  • Mengineyo: Kamera kuu ni ya Megapixel, f/1.75, ikisaidiana na nyingine ya Megapixel 12 (Laser/PDAF) 12 MP. Kamera ya selfi ni ya megapixel 20 (f/2.0, 0.9µm), pia simu inakuja na betri la mAh 4,000 na huku simu ikikubali hadi laini mbili (Laini za ukubwa wa Nano).
SOMA PIA  Njia Nne za Kuongeza Kasi ya Kompyuta au Simu Yako

Simu hii kwa sasa imeshatambulishwa nchini Uchina na itaanza kupatikana mara moja nchini humo kabla ya kuanza kusambaa kwenda kwenye mataifa mengine.

Bei: Toleo la diski uhifadhi wa GB 128 litauzwa kwa takribani dola 435 za Kimarekani – Tsh 1,000,000 , huku toleo la GB 256 likiuzwa kwa takribani dola 508 za Kimarekani – takribani Tsh 1,200,000/=.

SOMA PIA  Kwa nini uchague au usichague simu za iPhone (iOS) badala ya Android?

Vipi una mtazamo gani juu ya simu janja hii?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |