fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Apple IPhone simu

Kuwa Tayari Kwa IPhone Mini Kutoka Apple!

Spread the love

Inasemekana kampuni ya Apple, watengenezaji wa simu za iPhone na tablet za iPad wanauwezekano wa kutoa toleo dogo la iPhone kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Kutokana na vyanzo mbalimbali vya habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Apple, Tim Cook, ashaongelea suala hilo na moja ya kampuni kubwa ya mtandao wa simu huko Marekani, na hatua za mwanzo za utafiti tayari zishaanza.

Kama habari hizi ni za kweli, na hakika zina zaidi ya asilimia 90 ya kuwa kweli hii itakuwa inaonesha jinsibgani kampuni ya Apple inazidi kubadilika ili kuweza kuhimili ushindani. Kutoa iPad Mini mwishoni mwa mwaka jana kulionesha mabadiliko haya, kwani kwa muda mrefu kampuni hiyo ilishikilia msimamo wa kutokutoa toleo dogo la tablets zake maarufu za iPad.
Simu hiyo inasemekana inategemewa kuuzwa kati ya dola 100 hadi 150 za Marekani, ambazo ni takribani Tsh 160,000-250,000/=, na itakuwa ndogo kidogo kwa ukubwa kulinganisha na vipimo vya sasa vya iPhone 5 na zile zilizotoka kabla yake. Uamuzi huu kwa namna kubwa ni ili kuweza kushindana na smartphone/simu za bei rahisi zinazotumia Android hasa katika nchi zinazoendelea kama China na nyinginezo. Na kwa kutoa iPhone inayoweza kuuzwa kwa bei rahisi kwa asilimia kubwa kutasaidia kukuza mapato ya Apple na vilevile kuongoza asilimia ya umiliki wa soko linalozidi kuwa la ushindani zaidi, la simu.
Hivyo kama ulikuwa una nia ya kumiliki iPhone ila bei ikawa kikwazo basi vumilia kidogo, mambo mazuri yanaweza yakafika muda si mrefu!

*Vyanzo www.qz.com, verge.com na mitandao mingine!

SOMA PIA  Jinsi ya kuficha au kufichua mazungumzo kwenye WhatsApp
Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania