fbpx

Andorid Pie yaenea zaidi kuliko Oreo

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Leo hii ukinunua simu janja kwa mtu kama haipo kwenye toleo la Oreo (Android 8 au 8.1) basi inatumia Android Pie na kwa mujibu wa taarifa za mwaka huu kifikia mpaka mwezi Mei imeonekana toleo hilo la kenda kwa upande wa programu endeshi za Android yaenea zaidi kuliko ile ya nyuma yake.

Kila leo simu janja (rununu) zinazotumia mfumo endeshi wa Android zinatoka mpya, Oreo/Android 9 ndio zenye umaarufu kwa sasa hivyo basi hata pale rununu mpya inapotoka inakuwa imewekwa mojawapo ya matoleo hayo mawaili kwa upande wa Android. Toleo namba kenda (tisa) kwa mfumo endeshi wa Android umeonekana kuenea kwa kufikia 10%  ya simu zote za Android tangu kutambulishwa kwake mwezi Agosti 2018.

INAYOHUSIANA  Tegemea Kutumia Skype Kupitia Kivinjari Chako Tuu!

Kwa upande wa Oreo yenyewe iliweza kufikia 10% ya simu zote zinazotumia mwezi Julai 2018 ambapo ilitambulishwa kwa watu mwezi Agosti 2017 na mpaka kufikia Aprili 2019 ilikuwa imeenea kwa 12.1% pekee.

Hali ikoje kwa matoleo mengineyo ya Android?

Tunafahamu kuwa programu eneshi haikuanza leo wala jana na tangu huko nyuma imekuwa ikiboreshwa kwa toleo baada ya toleeo na unaweza kushangaa kuna simu za Android bado zinatumia toleo la kwanza kabisa kutoka lililobeba jina la programu endeshi husika.

yaenea zaidi

Android Oreo inachukua asilimia 28 ya simu zote za Android.

yaenea zaidi

Mchanganuo kuanzia toleo la Android, jina lake, asilimia ya simu inazotumika mpaka sasa na ukuaji wake tangu kuzinduliwa kwake mpaka mwezi Mei 2019.

Simu za Android ndio nyingi sokoni/zinazotumiwa na watu wengi na kuna zaidi ya simu janja bilioni 2.5 kwa idadi hivyo basi kila asilimia moja iliyoonekana inawakilisha simu 25 milioni ambazo zinatumia Android.

yanzo: GSMArena,  Android Central

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.