Mtandao wa kijamii wa Facebook unafanya majaribio mfumo wa kugundua watu ambao wanafungua akaunti feki, swala la akaunti feki limekuwa likiichafua sana Facebook kwa kipindi kirefu.
Mfumo huu utakapoanza kufanya kazi utawazuia watumiaji wote ambao ama wanatumia picha za watu wengine katika akaunti zao ama majina ambayo sio yao, hii ni taarifa mbaya kwa kina jokate feki na wamiliki wote wa parody akaunti za FB kwani mwisho wao umefika.
Naamini umeshawahi kukutana na matangazo kadhaa ya masupastaa wakisema kwamba akaunti fulani ya facebook sio yangu, hii ni moja ya vitu ambavyo vimekuwa ni vinainyima facebook kuwa na wateja wengi zaidi.
Kutumia jina ambalo sio lako ni kinyume na sera za majina za FB, kama wewe unatumia jina la mtu mwingine lazima ujue hii sio tu kinyume na sera za FB wenyewe lakini pia hii nikinyume na sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015.
Huduma hii itakuwa inawajulisha watumiaji pindi itakapo kuwa inaona kunamtu anajaribu kutumia taarifa zao kufungua akaunti nyingine, huduma hii itakuwa inafanya kazi kutegemea na taarifa kama vile majina na pia picha za profile.
Hii ni taarifa nzuri sana kwa baadhi ya mastaa wa kibongo ambao majina na picha zao zimekuwa zikitumiwa katika Facebook kwa minajiri ya kitapeli, lakini pia hii ni habari nzuri kwa watumiaji mtandao wa Twitter kwani nako swala la parody limekuwa linaotamizizi kwa kasi kubwa sana.
Teknokona inaendelea kuwasihihi watumiaji wa mitandao yote ya kijamii kutojiingiza katika vitendo vya kuiga ama kujifanya watu wengine, hili ni kosa kwa mujibu wa sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015.