Tukubali ukweli ni wachache sana huwa wanafurahia kupokea mialiko ya kucheza magemu Facebook, na huu utokana na ukweli hatupendi michezo hiyo au hatuwezi tuu kucheza michezo hiyo Facebook. Kwa kifupi tunatamani kama ingewezekana tumuambie mtu aliyetuma abakie na gemu zake kwani sisi hatuvutiwi nayo lakini tunashindwa.
Hakuna njia ya kuondoa mialiko hii moja kwa moja bali kuna njia ya kukuwezesha kuondoa kabisa mialiko mipya ya gemu fulani kutoka watu wote au kuondoa mialiko ya magemu kabisa kutoka kwa mtu flani. Na wengi tunajua kuna magemu flani flani ndiyo huwa tunapokea zaidi mialiko kupitia marafiki zetu. Fuata hatua hizi kuondokana kabisa na usumbufu huo;
1. Hatua ya kwanza ni kuwa Facebook, ingia kwenye akaunti yako. Kisha bofya kwenye alama ya
2. Ukibofya hapo chagua sehemu ya Mipangilio (Settings)
3. Kisha bofya kwenye ‘Blocking’ kama picha inavyoonesha
5. Nenda eneo lililoandikwa ‘Block App Invites’ na kisha andika jina au barua pepe ya mtu ambaye hutaki kupokea mialiko kutoka kwake. 🙂 Pia unaweza kuchagua kuondoa mialiko kutoka gemu au app yeyote ile kupitia kuandika jina la app hiyo kwenye ‘Block Apps’
Furahi sasa, mwisho wa kusumbuliwa na mialiko ya magemu au apps usizokuwa na mipango nayo umefikia mwisho! Kumbuka kusambaza makala yetu! #TupoPamoja
No Comment! Be the first one.