Na Brian L. Anderson
Dunia ya kompyuta-pakato au laptopu kwa lugha ya kisasa imepamba moto. Kila kampuni inapigania kujiweka tofauti na ushindani na tayari kampuni kama IBM zimejitoa kabisa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Chromebooks, Ultrabooks, na ‘hybrid’ zimejitokeza kutokana na jitihada za makampuni mbalimbali kulenga zaidi mahitaji na malengo yako mtumiaji. Kompyuta hizo zimefikia hatua ya kutaka kuondoa kabisa dhana ya laptopu kama tulivyoizoea. Muda si mrefu, utaaanza kuulizia madukani laptop ya aina fulani. Ni aina ya gani ya laptopu itakufaa wewe? Soma zaidi.
Wengi wanatazama Chromebooks kama jaribio la Google la kuleta kompyuta itakayotumika mahsusi kama kivinjari mtandao na hatimaye kuwa mbadala wa kompyuta za Windows kwenye suala la kufanyia kazi.
Chromebook zinaendeshwa na mfumo-endeshaji wa Chrome OS amabao umetokana na kivinjari wavuti cha Google Chrome. Kompyuta hizi zimeundwa kutumika wakati ikiwa mtandaoni. Data na programu zake nyingi, kama si zote hudumu kwenye ‘cloud’, ambayo ni sehemu maalumu mtandaoni kwa data.
Chromebooks zina mandhali ya Pixel zakuvutia zinazotengenezwa na Google wenyewe kwa chuma cha alumini.
Chromebooks nyingi zinauzwa bei chee sana, kuanzia $200 kwa Acer C720 ya inchi 11.6 hadi $300 kwa HP Chromebook 14 kubwa au Acer C720P yenye skrini ya kupangusa (touchscreen). Chromebooks zote hizi zinavutia na ni nyembamba na nyepesi.
Bei za Chromebook zinaweza kukupagawisha sana ila inabidi ujue mambo muhimu. Mosi, asili ya Chromebooks ni kivinjari wavuti. Itafanya kazi vizuri kabisa kama hautafungua madirisha mengi ya wavuti. Pili, Chromebook itakuodoa kwenye ulimwengu wa Windows – hii ina maana utaepukana na hofu ya virusi ulivyozoea na utakuwa huna haja ya ku-update laptopu yako. Kimsingi, Chromebooks zinarahisisha suala zima la kutumia kompyuta.
Chromebooks zinazaweza kufanya vitu vichache isipoungwa na mtandao. Uwezekana kutunga barua pepe, unaweza kuangalia na kuhariri “spreadsheets”, nyaraka, “presentations” na michoro lakini kamwe hutapata mafaili mengine ambayo yalikuwa ‘uploaded’ na kutunzwa kwenye Google. Pia, usipokuwa mtandaoni, hautakuwa na uwezo wa kugawa, kuhamisha au kufuta mafaili yoyote kwenye Google Drive.
Ni muhimu kutambua kuwa Chromebooks haziwezi kufanya mambo mengi amabayo pengine ungeyataka ufanye bila mtandao, hasa wale wa wanotumia programu za Windows kwa ajili ya kazi, biashara na zaidi. Kwa mfano, hakuna njia ya kujenga au kuhariri maingizo ya kwenye kalenda, au hata kuangalia kazi zilizowekwa awali.
Pia huwezi kuweka printer yoyote tu ikafanya kazi. Kama unahitaji kuchapa mara kwa mara, itabidi, aidha uunge printer iliyowezeshwa na Google Cloud Print au utumie kwa kompyuta nyingine mtandaoni. Chromebooks hazitumii kabisa CD.
Ultrabook ni jina la mauzo(brand) na pia aina ya laptopu za hali ya juu kabisa ambazo sifa na viwango vyake hutolewa na kampuni ya Intel. Sifa kubwa ya Ultrabook ni uwembamba pamoja na kuwa na betri inayokaa na chaji muda mrefu. Kimsingi, ukitaja Ultrabooks umaaanisha laptopu zenye nguvu lakini potabo.
Ultrabooks zinatumia Windows, hivyo basi, Intel inajibu mapigo kwa Apple, inayotengeneza MacBook Air na kampuni hiyo imeamua kuhaikisha hadhi ya hizi laptopu inabaki juu kama au kuzidi MacBook kwa kudhibiti viwango vyake.
Ultrabooks zilizotolewa hivi karibuni huwa na prosesa ya Haswell na unene wa chini ya inchi 0.9, huwaka kwa haraka sana, huhimili masaa sita ya video ya HD, huwa na skrini ya kupangusa (‘touch-screen’), teknolojia ya Wireless Display na huweza kuaamrishwa kwa sauti.
Hybrid, kompyuta mseto…au chochote unachotaka kuuita, ni kompyuta unayoweza kuitumia kama laptop au kama tableti ukitaka. Kompyuta hizi zenye touchscreen na keyboard za kuchomoa zinatengenezwa kwa prosesa ya Intel Core.
Kuna aina mbili ya kompyuta hizi – Zile zinazoelekea upande wa laptopu zaidi (kama Lenovo IdeaPad Yoga 11s au Dell XPS 12) ambazo kimsingi ni Laptops zenye skrini ya kugeuzika ili kuzifanya kuwa kama tableti na zinazoelekea ki-tableti zaidi na huwa na keyboard za kuchomoa. (Kama Microsoft Surface).
Hybrid za ki-laptopu zaidi huwa na bei ya juu zaidi ya laptopu za kawaida. Touchscreens kwenye hizi laptopu huathiri uwezo wa betri, hasa kwa zile zisizotumia prosesa ya “Haswell” au “Bay Trail” Atom. Hybrid zote ni kubwa na nene ukilinganisha na tableti ya kawaida, hasa zile zilizoelekea ki-laptopu zaidi kwa hiyo, hybrid zinafaa hasa zikipakatwa, hata kama unazitumia kama laptopu.
Hatima:
Chromebook ni nzuri kwa mtu wa kawaida anayependelea zaidi kukaa mtandaoni na kutumia huduma na programu za mtandaoni. Ni kompyuta ambayo utapata kwa bei chee.
Laptopu za Windows, iwe ni Ultrabook au Hybrid, ni kwa kutumia mtandao na kutumia programu kedekede bila kuwa mtandaoni na kufanya kazi zako kwenye Microsoft Office, kuunganishwa na mitandao mahali pa kazi, kwa kutumia programu mbalimbali, kuhariri picha na video mtandaoni na bila mtandao, kuongea na rafiki yako aliopo Afrika ya Kusini au popote duniani kwa Skype, kuhifadhi CV yako kwa Cloud au kwenye diski yako na kushusha magemu kedekede kutoka mtandaoni, kama FIFA 14, Need For Speed Rivals, na mambo mengi uliyozoea kwenye kompyuta ya kawaida.
No Comment! Be the first one.