fbpx

Toshiba Wakuletea Tableti ya Window 8.1 kwa Tsh Laki 2

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Microsoft amekuwa akipata ushindani sana kibei kutengeneza tableti ya bei ya chini kuweza kushindana na zile za Android ambazo zipo kibao kwa bei ya chini. Kupitia ushirikiano na kampuni ya Toshiba Microsoft wameweza kuziba ilo pengo, Encore Mini ni tableti yenye uwezo wa kawaida kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya kila siku imeingizwa sokoni na kampuni ya Toshiba kwa bei ya dola za kimarekani 119 ambazo ni takribani Tsh198,000/=

Je Inavutia?

Kamera ya Nyuma

Kamera ya Nyuma

Ingawa ukichunguza sana unaweza pata tableti za Windows 8 kwa bei kama hiyo au chini kidogo, nyingi zake ni zilizotengenezwa na makampuni yasiyo makubwa ni tableti zilizo nene na hazipo kwenye ubora sana. Toshiba ni jina linalokubalika na ni moja kati ya makampuni makubwa ya vifaa vya elektroniki, kupitia Encore Mini Toshiba wamejitahidi kubana matumizi katika utengenezaji ila kwa wakati huo huo bila kupoteza ubunifu na ubora kwa kiwango flani.

INAYOHUSIANA  Second Skin: Wanasayansi waja na Ngozi ya Bandia, Kuficha Uzee na Makovu!

Encore Mini ni tableti inayotegemewa kununuliwa na wengi waliowapenzi wa Windows 8 na walikuwa wanajikuta wakichagua tableti za Android kwa ajili ya urahisi wa bei wa tableti hizo. Tableti ya Encore inakuja na programu ya Microsoft Word, ila ni kwa leseni ya mwaka mmoja tu, baada ya hapo kama utataka kutumia programu hiyo kwa matumizi makubwa basi itabidi ulipie.

Sifa za Encore

 • Ukubwa – Inchi 7
 • Sifa za kioo (display) – 1024×600 pixels
 • Windows 8.1 ‘with Bing’
 • Inakuja na programu ya Office 365 ikiwa na leseni ya Mwaka 1.
 • Prosesa – Intel® Atom® Processor Z3735G (2MB Cache, Up to 1.83GHz)
 • RAM – GB 1
 • Diski Uhifadhi – GB 16
 • Kamera ya Mbele 0.3MP (ina Microfoni pia)
 • Kamera ya Nyuma 2.0MP
 • Inatumia kebo ndogo za USB (Micro-USB 2.0)
 • Inasehemu ya kuingiza kadi ndogo za uhifadhi zenye ukubwa wa hadi GB 128 (Micro SD)
 • Ina Wi-Fi® Wireless networking (802.11b/g/n) na Bluetooth® v 4.0
 • Bluetooth® v4.0
 • Muonekano wa rangi nyeupe kwa nyuma
Muonekano wa Sehemu ya Kuwekea kadi na mengineyo

Muonekano wa Sehemu ya Kuwekea kadi na mengineyo

Je ushawahi au unatamani kumiliki tableti ya Windows 8.1? Tupe sababu zako….

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

4 Comments

 1. Habari Ayaru, kwa sasa bado hatupata taarifa za wapi tableti hizi zinapatikana kwa Tz, ila tukifahamu tuu tutakufahamisha. Kumbuka kuandikisha anuani yako ya barua pepe ili kupata mawasiliano zaidi. Asante

Leave A Reply