Kampuni ya Apple yaelezea rasmi ya kwamba simu zao za iPhone zimetengenezwa kuweza kudumu katika matumizi kwa angalau miaka 3 kabla ya kuitaji kubadilishwa, huku kompyuta zao za Mac zinatakiwa kutumiwa kwa kipindi cha miaka minne tu.
Katika data waliyoitoa inayoonesha mahusiano ya teknolojia ya vifaa vyake na masuala ya utunzaji wa mazingira imeonesha data zao zikionesha mategemeo ya muda wa utumiaji wa vifaa vyake.
Ingawa data hizo hazijasema kwamba vifaa vyake vita’expiry baada ya muda flani ila data hizo zinaonesha mategemeo ya Apple kuhusu muda wa kutumika kwa bidhaa zao zinapoingia rasmi sokoni.
Ukweli ni kwamba labda hiyo miaka 3 ya iPhone ni kwa mtumiaji wa kwanza, watumiaji wengi wa nchi zinazoendelea huwa tunasubiria kununua zilizotumika kwa watu na sisi tunatumia kwa muda mrefu tuu – na hivyo kukuta iPhone moja inaweza ikawa inatumika kwa ata miaka 6 – 7.
Expiry date? – Labda miaka ya baadae, lakini kwa sasa vifaa kama simu na kompyuta vinaweza tumika kwa miaka mingi tuu – havina expire data. 🙂
Kwa upande mwingine siku hizi inaonekana ata Apple wamegundua ya kwamba kuna matoleo ya zamani ya simu zake za iPhone bado yanatumika kwa sana, ili linaoneshwa na uamuzi wao wa kuendelea kutoa masasisho (updates) ya matoleo mapya ya iOS kwa simu za zamani tuu – kama iPhone 4s.
Bado iPhone nyingi za zamani zinatumika!
Data kutoka IHS nchini Marekani zinaonesha katika simu za iPhone zinazotumika – Asilimia 29 ni matoleo ya iPhone 5, asilimia 23 ni iPhone za zamani kabla ya iPhone 5 – iPhone 5 iliingia sokoni Septemba mwaka 2012.
Kwa data zao pia wanategemea vifaa kama kompyuta za OS X na tvOS (Apple TV) kutumika kwa miaka 4 na wakati vifaa kama saa zao janja (WatchOS) na vya iOS (iPhone na iPad) ikiwa ni miaka 3.
Kwa kiasi kikubwa inaonekana siku hizi watu ni wagumu zaidi kubadilisha vifaa kama simu au kompyuta mara kwa mara – hii inatokana na sababu mbalimbali moja ikiwa siku hizi kunatofauti ndogo sana ya vifaa vipya hasa hasa kwenye eneo la ‘Specs’. Kwa wengi kutoa pesa kubwa kwa ajili ya kununua kipya chenye tofauti ndogo na kile kilichotumika (used) kinachouzwa kwa bei nafuu limekuwa ni jambo gumu.