Mawasiliano kwa njia ya barua pepe yamekuwa yakisaidia uharaka wa kupata majibu/kujuliana hali tofauti na mtu akitumia njia ya kutuma barua kwa njia ya Posta (ingawa daima barua za kuandikaina kisha kupata majibu baada ya muda fulani zitabaki kuwa na heshima yake 😉 😉 ).
Ingawa siku hizi kuna Telegram, WhatsApp na nyinginezo lakini njia ya barua pepe ina raha yake sana tuu hasa kama ni mtu unayependa kutunza kumbukumbu katika mpangilio fulani. Wengi wetu tunaweza kuwa tunatumia barua pepe kulingana na mahitaji ya kzi zetu au uharaka wa kutaka kupata majibu kwa wakati.
Si ajabu kabisa kwa wale ambao tunapenda kufanya kazi mahali popote, wakati wowote hivyo tunaweza kuandaa kile ambacho tunataka kumtumia mtu kwa njia ya barua pepe leo lakini kikatumwa kesho saa fulani wakati huo wewe unakuwa haujaingia kwenye akaunti yako kufanikisha hilo lakini teknolojia imesaidia kufanikisha kinachohitajika kufanyika.
Fanya hivi kuweza kutuma ujumbe wako kwa njia ya barua pepe (Gmail) wakati ambao utapenda uutume
Hatua ya kwanza: Baada ya kumalia kuandika kile ambacho unataka kutuma kwenda kwa mhusika kwenye Gmail iwapo umetumia kompyuta basi badala ya kubofya kitufe kilichoandikwa “Send” wewe sogeza kiteuzi pembeni kidogo kisha bonyeza ule mshale ulioelekea juu halafu chagua “Schedule to send“.
Hatua ya pili/tatu. Ukurasa mdogo utafunguka ambapo mhusika anaweza kuchagua ujumbe ule utumwe saa 2 asubuhi, saa 3 asubuhi, ya tarehe husika au ukaweza kuchagua tarehe/saa (pick time & date) ambayo utataka ujumbe huo umfikie atakeyeupokea.
Vipi kwa upande wa simu?
Kutokana na kupanuka kwa teknolojia vitu vingi ambavyo vinaweza kufanyika kupitia kwenye kompyuta basi hata ndani ya simu janja jambo hilo linawezekana pia. Unaptaka kutuma ujumbe wako kwa njia ya barua pepe kupitia simu janja sasa badala ya kubonyeza kile kitufe cha mshale unaoangalia upande wa kulia bonyeza zile nukta 3, menyu ndogo itatokea na hapo utachagua “Schedule to send” kuchagua muda/tarehe au kupanga ya kwako mwenyewe ambapo ujumbe utatumwa.
Baada ya kumaliza kupanga muda/tarehe amabyo ujumbe utatumwa ni lazima kubofya kitufe kilichoandikwa “Schedule to send” ama kwa tafsiri isiyo rasmi “Panga kutuma”. Lakini daima tukumbuke kwamba shughuli inawezekana tu kwa tarehe ya siku husika na si siku ambayo imeshapita (jana, juzi, n.k).
Vyanzo: The Verge, mawazo binafsi
No Comment! Be the first one.