fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta

Windows 10 Sasa Katika Kompyuta Milioni 110! #Windows10TZ

Windows 10  Sasa Katika Kompyuta Milioni 110! #Windows10TZ

Spread the love

Ni takribani miezi miwili tokea programu endeshaji ya Windows 10 kuanza kupatikana kwa watumiaji wote, na sasa data inaonesha kuna takribani kompyuta milioni 110 zinatumia programu endeshaji hiyo.

Pia mtu yeyote anaweza kutembelea mtandao wa Microsoft na kutumia Windows 10 kwenye mtandao kwa majaribio bila kupakua kwenye kompyuta

Ili kuzidi kufanya watu wajaribu programu endeshaji hii. Mtu yeyote anaweza kutembelea mtandao wa Microsoft na kutumia Windows 10 kwenye mtandao kwa majaribio bila kupakua kwenye kompyuta

Idadi imepungua kudogo ukilinganisha na uwezo wa kuwa kwenye kompyuta milioni 75 ndani ya mwezi wa kwanza wa kuanza kupatikana. Hii ikimaanisha katika mwezi wa pili kompyuta milioni 35 ndio zimeongezeka. Lakini bado idadi ya milioni 110 ndani ya miezi miwili ni kubwa sana na inastaili pongezi.

Kujaribu bila kupakua programu endeshaji ya Windows 10 basi tembelea – http://wndw.ms/b9HlhD

Idadi hii inafanya idadi nzima ya kompyuta zinazotumia Windows kuwa ni asilimia 6.42 ya kompyuta zote duniani. Na hii inatokana na ukweli ya kwamba toleo hili si la bure kwa wote na kwa kiasi kikubwa bado utumiaji wa Windows XP ni mkubwa na watumiaji hao hawana sifa ya kupata toleo la Windows 10.

Pia makampuni yenye sifa ya ‘Enterprises’ yanayopata huduma spesheli ya kuwekewa toleo la Windows 10 bado programu ya kuwahamisha kutoka matoleo ya zamani kuja hili jipya bado haijaanza. Watumiaji wenye sifa ya ‘enterprises’ wanatengeneza asilimia 10 ya kompyuta zote zinazotumika kwa sasa.

SOMA PIA  Microsoft yalipa faini ya $10,000 kutokana na kulazimisha Windows 10!

Je ushajaribu toleo la Windows 10? Unaweza kufuata hatua nyepesi katika mtandao wa Microsoft kuweza kupata toleo la Windows 10 – Bofya http://wndw.ms/DlmeQn . Pia unaweza kusoma chambuzi zetu mbalimbali za Windows 10 kwa kubofya – http://teknokona.com/tag/windows-10/

Vyanzo: http://www.iusbpreface.com na http://www.theinquirer.net

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania