fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Picha Sayansi

Adobe Kwa Ushirikiano Na Stratasys Wanaleta ‘3D Printing’ Katika Photoshop!

Adobe Kwa Ushirikiano Na Stratasys Wanaleta ‘3D Printing’ Katika Photoshop!

Spread the love

Kampuni la Adobe na Stratasys yametangaza rasmi ushirikiano wao ambao utaleta mabadiliko makubwa haswa kwa wataalamu wa ubunifu duniani. Stratasys ni kampuni linalozalisha printa za 3D (3 Dimensions)

Photoshop ni program inayomilikiwa na Adobe ambayo unaweza ukafanya nayo vitu vizuri, vya kuvutia na saa zingine visivyoelezeka — Binafsi, naikubali sana —  Pia ni program inayotumika sana duniani katika masuala ya picha kama vile kuzihariri (Edit) N.k

Kampuni Ya Stratasys Ikijumuika Na PS (Photoshop) Ile Ya Adobe Chini Yake Ikionyeshwa Baadhi Ya Kazi ZIlizo Katika Mfumo Wa 3D

Ushirikiano huu ulitangazwa katika Adobe MAX 2015 iliyofanyika huko Los Angles marekani. Na Kizuri kuhusu ushirikiano huu kwa watumiaji ni kwamba utawahi kuanza. Pia ushirikiano huu umekuaja baada ya mwaka tangia kampuni la adobe lifanye maboresho kwenye Adobe Creative Cloud juu ya swala la 3D. Hii inamaanisha kuwa maboresho hayo yalikuwa kwamba, watumiaji wangeweza kufanya ubunifu wao wa 3D na kisha kuupeleka katika mafaili yenye mfumo wa 3D bila kuwa na shida yeyote.

Ushirikiano huu utajikita sana katika kuhakikisha matumizi ya 3D printing yanafanyika haswa kwa watumiaji wa Adobe CC. Kutokana na hili watumiaji watakuwa na uwezo wa kutuma mafaili yao ya 3D kwa ajili ya kutengenezwa kupitia ‘Stratasys Direct Express’

Pia kampuni ya adobe inatafuta njia ya aina yake katika swala zima la 3D. Tegemeo lake ni kupata njia ambayo itawezesha au italeta uwezekano wa kubeba rangi kama ilivyo katika ubunifu na kuipeleka mpaka katika hatua ya mwisho (ikiwa ime’print’iwa) bila kupoteza uhalisia wowote. Hii yote itakuwa ni muhimu kwa wale wanao ‘print kwa kutumia mfumo huu wa 3D na kwa sasa hata rangi zinakuwa kidogo hazipo katika uhalisia katika mfumo wa ku ‘print’ kwa 3D

Muonekano wa Picha  Ya Mfumo Wa 3D Katika Programu

Muonekano wa Picha Ya Mfumo Wa 3D Katika Programu

Kumbuka kampuni la Adobe na hili la Stratasys wana lengo sawa, Lengo hilo ni kuwapatia watumiaji wake uwezo wa hali ya juu unaohisiana na maswala ya ‘3D printing’ na pia kuwawezesha kutengeneza vitu vya kibunifu ambavyo hakuna mtu aliyeweza fanya.

SOMA PIA  FAHAMU: Mega Pixel (MP) Ni Nini Na Inafanya Nini Katika Picha!

Siku hizi makampuni mengi makubwa yanaungana ili kuhakikisha yanaleta mambo makubwa na yenye faida hasa kwa watumiaji wake . Teknolojia inakuwa na watu wanajaribu kulitumia hilo kuleta mambo mapya ya kibunifu. Tuambie wewe unaonaje hili, ni jambo jema sio? Tuandikie sehemu ya comment. Usisahau kutembelea mtandao wako namba moja wa TeknoKonaDotCom. TeknoKona Tupo Nawe Katika Teknolojia

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania