Katika miaka ya karibuni kampuni ya Google ilinunua teknolojia na huduma mbalimbali, moja ya manunuzi waliyoyafanya ni pamoja na Nik Software. Kampuni inayomiliki app na programu mbalimbali za uboreshaji na ubunifu wa picha.
Google walinunua kampuni ya Nik Software mwaka 2012. Nik Software wakati huo walikuwa wanamiliki app maarufu katika iOS ya Snapseed na baada ya ununuzi huo muda si mrefu toleo la app ya Snapseed kwa ajili ya Android likafuata.
Pia Nik Software walikuwa nauza kifurushi cha programu mbalimbali kwa ajili ya masuala ya ubinifu ya picha (kama vile Adobe Photoshop) – wakati Google wananunua kampuni hiyo kupata programu hizo zote kwa ajili ya kompyuta – Windows na Mac, ilikuwa inagharimu dola 499.95 ila Google wakatengeneza kifurushi cha programu zote na kushusha bei hiyo hadi $150.
Kwa kuwa Google ni maarufu kwa huduma zake nyingi ambazo ni za bure – Nik Collection imekuwa kwa muda mrefu huduma inayotia doa sifa hiyo. Na sasa Google wameamua kufanya programu hizo bure kwa watumiaji wote.
Kama wewe ni mtumiaji wa programu za kompyuta kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya kimuonekano ya picha basi utakuta programu hizi za Nik Collection zinakidhi mahitaji mengi tuu mithili ya zile za Adobe.
Snapseed | Google Play | App Store (iOS)
Nik Collection | Mac & Windows
chanzo: Google