fbpx
Anga, Teknolojia

Aliyetarajiwa kuwa Mwafrika wa kwanza mweusi kwenda angani afariki

aliyetarajiwa-kuwa-mwafrika-wa-kwanza-mweusi-kwenda-angani-afariki-dunia
Sambaza

Mandla Maseko, DJ wa zamani wa Afrika Kusini ambaye alitarajiwa kuwa mwafrika wa kwanza mweusi kufanya safari ya kwenda pasipoonekana kwa macho ya kawaida afariki kwa ajali ya pikipiki kabla ya kutimiza ndoto yake.

Mandla Maseko aliyekuwa askari wa jeshi la anga la Afrika kusini, mwenye umri wa miaka 30, alikuwa mmoja wa watu 23 walioshinda safari ya kwenda angani kwa udhamini wa chuo cha anga cha Marekani, Axe Apollo Space Academy.

Marehemu alikuwa akifikiri kuwa katika maisha yale angeweza kufikia kuwa askari au mwanasheria lakini si mtu aliyefunzwa jinsi ya kuiongoza ndege halikadhalika na mambo mengine yanayohusiana na anga za juu. Wakati fulani alipokwenda kwenye kambi ya wana anga akaamini kuwa inawezekana kuwa na ujuzi kwenye fani hiyo.

kwenda angani
Mandla Maseko alipata nafasi ya kwenda angani baada ya kuwashinda washiriki milioni 1 kutoka mataifa 75 duniani mwaka 2014.

Alifanikiwa kuwa rubani wa kujitegemea lakini pia askari wa cheo cha “Corporal” kwenye jeshi la ulinzi Afrika Kusini. Kifo cha Bw. Mandla kimeondoa  historia kuandikwa  kwa Mwafrika wa kwanza mweusi lakini pia angekuwa Mwafrika wa tatu baada ya Mark Shuttleworth (2002) na Mike Melvill (2004) kwwwenda anga za mbali.

INAYOHUSIANA  Firefox Send: Mozilla waja na huduma ya kutuma mafaili kwa usiri

Mtu wa kwanza mwafrika kwenda kwenye anga za mbali ni Mwafrika Kusini mweupe na mfanyabiashara, Bw. Mark Shuttleworth mwaka 2002 kwa chombo kilichotengenezwa na Urusi aliyelipa pauni 12 milioni sawa na zaidi ya $15 milioni na kukaa kwenye kituo cha kimataifa kilichopo angani kwa muda wa siku nane.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.