NASA imefanikiwa kukipata chombo chake ambacho kilipotea miaka miwili iliyopita kikiwa katika shughuri za kitafiiti, Wakala huu wa usafiri wa anga nchini Marekani wanasema kwamba wameweza kurudisha mawasiliano na STEREO B jumapili hii.

STEREO B ilikuwa ni kati ya vyombo viwili ambavyo vilikuwa vinafanyia utafiti uhusiano kati ya Jua na Dunia, Chombo kingine kilipewa jina la STEREO A na wakati STEREO B inapotea wanasayansi walikuwa wanazifanyia majaribio timers zake.
Je, nini kilitokea mpaka chombo hicho kupotea?
Kilichotokea ni kwamba wakati wanasayansi hao wakiwa katika kazi hiyo ya majaribio chombo hicho kilisogea na kukaa nyuma ya Jua hivyo kuondoka katika eneo ambalo kuna mawasiliano.
CNN imeripoti kwamba Chombo hiki kimepatikana kwa msaada wa kundi la antena ambazo zimefungwa kwaajiri ya kuchunguza tabia za sayari mbalimbali.Ingawa chombo hicho kilipoteza mawasiliano lakini kimekuwa kikiendelea na kazi zake vizuri kwa miezi 22 mpaka ambapokimepatikana.