Kampuni ya Marekani ya Orion Span Inc ya imetangaza mpango wa kujenga hoteli ya kwanza ya anga ya juu iitwayo ‘Stesheni ya Aurora’.
Mpango huo bado uko kwenye kipindi cha kukusanya uwekezaji, lakini sasa watu wanaweza kuweka nafasi safari ya kwenda hoteli hii kwa kulipa dola za kimarekani elfu 80 kama amana ya kwanza.
Hoteli hii itakuwa na vitengo kadhaa ambavyo kila kimoja kina urefu wa mita 13 na upana wa mita 4; ukubwa wa vyumba vya hoteli hii utakuwa karibu sawa na ukubwa wa ndege aina ya Gulfstream G550.
Hoteli hii itaweza kupokea watalii wanne na wafanyakazi wawili kwa wakati mmoja.
Nnini ambacho watalii watakuwa wanakifanya kwenye hoteli ya angani?
Habari zinasema kwenye hoteli hii watalii watapata kuishi kama wanaanga, kuhisi ukosefu wa nguvu za mvutano wa dunia, kupiga picha ya dunia. Gharama ya kulala kwa siku 12 ni $9.5m|Tsh 21,375bn.
Vilevile, watalii hao wataweza kufanya majaribio ya kisayansi, kupanda mboga, kutazama mwanga aina ya Aurora na kutazama Mawio na Machweo kwa zaidi ya mara 10 ndani ya siku moja. Lakini kabla ya kwenda hoteli hii, watalii watahitaji kupata mafunzo kwa miezi mitatu.
Hoteli hii itasafiri kwenye mzingo ulioko kilomita 320 juu ya Dunia na kuzunguka mzingo mmoja kila baada ya dakika 90.
Sayansi na teknolojia ndio hiyo. Siku zote ulijua tu hoteli zinajengwa ardhini, katika miaka ya hivi karibuni tunafahamu kuwa ipo hoteli iliyojengwa chini ya maji na sasa ni angani. Sijui tunaweza tukaishukuru teknolojia/sayansi, majibu unayo wewe.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.