Foleni, foleni, foleni! Mara zingine zinakera sana na pengine mtu anaweza akaghairi kitu ambacho alitaka kukifanya kisa urefu wa foleni (kamba).
Nissan wameliona hilo na wamekuja na teknolojia (ProPilot Chair) ya kuweza kurahisisha jambo hili, haimaanishi kuwa hakutakuwa na foleni. Itakuwepo kama kawaida ila itakuwa haichukizi kama awali.
Kumbuka kuna watu wengi sana wanapoteza muda wao mwingi kusubiria vitu (wahudumiwe) katika foleni mbalimbali. Hivi unajua ‘Apple Store’ zinakuaga na foleni kubwa kiasi gani pale simu mpya zinapotoka?. Acha hiyo kitu kabisa, watu huwa wanalala pale kwa siku kadhaa.
Nissan wamekuja na Teknolojia ya kiti ambacho wamekiita ‘ProPilot Chair’. Kiti hichi kina uwezo wa kujiendesha chenyewe (pata picha ukiwa kwenye foleni kitaweza kukusogeza mbele (kwenye huduma).
Kiti janja hiki kina uwezo wa kusogea na kukifuata kiti chenzie kikisogea katika mstari mmoja (hakitatoka katika huu mstari).
Teknolojia hii kwa mara ya kwanza kabisa kabla haijafika katika viti kampuni ya Nissan ilikua ikiitumia katika magari yake yanayojulikana kama ‘Serena Minivan’ huko Japan.
Kampuni imeona ikuze zaidi teknolojia hii hata kwa vitu vingine amabavyo vinarahishisha maisha ya watu kila siku kama vile viti.
Kumbuka vile vile ukiachana na swala zima la foleni tuu viti hivi vina manufaa sana, kumbuka kuna watu ambao kwa namna moja au nyingine kutembea au kusimama kwao ni kitendawili mfano walemavu na wazee. Wakiwa katika viti janja hivi basi zoezi zima linarahishishwa.

Tazama Video Kujionea Namna Vinavyofanya Kazi.

Kwa sasa viti janja hivi (ProPilot Chair) vinafanyiwa majaribio toka tarehe 27 mwezi wa 9 mpaka tarehe 27 mwezi wa 12 mwaka huu (2016).
Kwa mtazamo wako niambie viti kama hivi vinaweza saidia sana katika mambo gani, ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini sehemu ya comment.