fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti

Kitufe cha ‘Like’ cha Facebook Kuboreshwa Zaidi: Emoji za Hisia Kuongezwa

Kitufe cha ‘Like’ cha Facebook Kuboreshwa Zaidi: Emoji za Hisia Kuongezwa

Spread the love

Sasa watumiaji wa Facebook hawatalazimika kuchagua LIKE katika posti za marafiki zao Facebook, na badala yake wataweza kuchagua Kupenda, Kuchukia, Kucheka, Kushangaa au kuhuzunika kwa kutumia Emoji mpya za hisia zitakazoambatanishwa katika marekebisho makubwa ya kitufe cha Like yanakayofanywa na Facebook.

Hayo yalitambulishwa jana na mwanzilishi wa mtandao huo, Mark Zuckeberg kupitia ukurasa wake wa Facebook, akiweka video iliyotambulishaujio wa vitufe hivyo vipya vinavyotazamiwa kuwa na nguvu kubwa kwa watumiaji wa mtandao huo.

Button hizi zimeongezwa kutokana na mapendekezo ya watui wengi kuwa na vitufe mbadala vya LIKE

Button hizi zimeongezwa kutokana na mapendekezo ya watui wengi kuwa na vitufe mbadala vya LIKE

“Tumechunguza aina ya comments na hisia zinazoonyeshwa kwenye posti mbalimbali na kugundua kuwa zainafanana ulimwenguni kote. Watu wote wanacheka, kuchukia, kushangaa n.k. Sasa tutawawezesha waweze kuonyesha hisia zako kwenye kurasa zao za Facebook.” Anaelezea Chriss Cox, mkuu wa bidhaa za Facebook.

Vitufe hivi vitakuwa vinatambulika katika tamaduni zote Ulimwenguni kwa sawa, ili kuwezesha wote kuwa na hisia za aina moja wakati  wa kuchangia katika posti za marafiki wote duniani.

Sasa mfumo huu unafanyiwa majaribio nchini Ireland na Hispania

Sasa mfumo huu unafanyiwa majaribio nchini Ireland na Hispania

Watu wengi wamekuwa wakisubiri Facebook walete vitufe vitakavyoweza kuonyesha hisia tofauti za zile za kitufe cha LIKE pekee, ili kuonyesha hisia hasi kama kuchukia, kuhuzunika au kucheka.

SOMA PIA  BlackBerry yapata faida: Mapato ya biashara zake yazidi kukua

Kwa wakati huu, vitufe hivi vya hisia vitapatikana kwa majaribio kwanza katika nchi za Spain na Ireland, kama kukiwa na mafanikio zitaachiliwa kwa Ulimwengu mzima.1444339907707

Baada ya saa 11 ya kuchapisha video hiyo kutambulisha vitufe vya hisia mtandaoni, zaidi wa watu Laki Tisa walipenda posti hiyo ya Zuckerberg, ishara tosha kuwa unasubiriwa kwa hamu na kukubalika kwa jamii.

SOMA PIA  Tovuti maarufu ya ExtraTorrent yaacha kupatikana

Watumiaji wa Facebook sasa wateweza kuchagua labda Kupenda, Kushangaa, Kuhuzunika au Kuchukia katika posti za rafiki zao. Haya ni zaidi ya walichopendekeza, kwani mwanzo walipendekeza kitufe cha Dislike kiongezwe kama tulivyochapisha siku za nyuma katika mtandao huu.

Huu ni mfululizo wa maboresho makubwa yanaoendelea kufanywa na Facebook baada ya kutambulishwa kwa mifumo mingi mipya ya mtandao wa Facebook, ili kuendelea kuongeza idadi ya watumiaji duniani.

Comment

Comments

  1. […] Tulishaandika kuhusu mipango ya mtandao wa Facebook kuleta Emoji mpya ili kuzidi kuongeza vionjo nje ya kitufe cha ‘LIKE’ kilichokuwepo kwa muda mrefu. Emoji hizo zaanza kupatikana. […]

  2. […] Tulishaandika kuhusu mipango ya mtandao wa Facebook kuleta Emoji mpya ili kuzidi kuongeza vionjo nje ya kitufe cha ‘LIKE’ kilichokuwepo kwa muda mrefu. Emoji hizo zaanza kupatikana. […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania