Kufua, kukunja na kupanga nguo si kazi inayopendwa sana na watu wengi tuu, yaani huwa wanaifanya kwa kua ina walazimu na wala si kwa kuwa wanaipenda. Ila pia wapo wanaopenda.
Katika kuonesha jinsi gani teknolojia inaweza kutumika kuzidi kuraisisha maisha ya watu wasiopenda shughuli hii kampuni ya Panasonic na wadau wengine wamefanikiwa kutengeneza roboti ya kwanza duniani kwa ajili ya kazi hiyo.
Laundroid ni robot anayeweza kupokea nguo, na kuzifua na kuzikausha na kisha kuzikunja na kuzipanga kulingana na aina ya nguo husika.
Laundroid inatengenezwa nchini Japani na kampuni ya Panasonic kwa ushirikiano na makampuni mengine ya nchini humo, Japani.
Inakadiriwa kwa wastani mtu anatumia takribani masaa 18,000 ambayo ni zaidi ya siku 375 za uhai wake kufanya kazi ya kukunja nguo, yaani ni takribani mwaka mmoja. Wanasema teknolojia hii itaweza kukusaidia kupata mwingine katika maisha wa kufanya mambo mengine.
Kwa sasa mashine hiyo inauwezo wa kupokea na kukunja nguo ndani ya dakika 5, na wanasema maboresho bado yanaendelea na hii ikiwa ni pamoja na kuiwezesha kufanya mengine hii ikiwa ni pamoja na uwezo wa kufua na kukausha nguo ndio kisha ikunje na ata kuweza kupanga kwenye sehemu husika.
Kimuonekano ni kama vile kabati kubwa, na nia yao ni kwamba mashine hii iweze kujengewa katika nyumba baadae huku mfumo mzima ukiunganishwa na makabati ili kuifanya iweze kuzipanga nguo baada ya kuzifua na kuzikunja. Leo kuu ni kwamba mtumiaji aweze kutupia nguo zake ndani yake usiku na kuiacha mashine ifanya kazi usiku kucha na kuweza kujizima yenyewe baada ya kumaliza kazi nzima hii ikiwa ni pamoja na kuzipanga kwenye mfumo mzima wa makabati uliounganishwa nao.
Laundroid yenye uwezo wa kukunja nguo tuu itaanza kupatikana kuanzia mwaka 2016 wakati yenye uwezo mzima wa kufua, kukunja na kupanga kwenye makabati utaanza kupatikana mwaka 2019.
Teknolojia inazidi kutumika katika kuzidi kuokoa muda ambao unaweza kutumiwa kufanya mambo mengine, je una maoni gani juu ya teknolojia hii?
Angalia video
One Comment