UnakuMbuka kipindi kilichopita BlackBerry ndio ilikua simu yenye kiki hasa katika App yake ile ya BBM (Blackberry Messenger). Nakumbuka baadhi ya marafiki zangu walikuwa hawataki kabisa kuuza simu zao. Yaani kwa kifupi simu hiyo ilikua na kiki kama unavyoona leo Samsung Galaxy na iPhone zinavyofanya vizuri
Baada ya soko kushuka na kupata na ukimya wa muda kidogo katika soko la simu, Blackberry inajipanga kurudi mwakani. Kipya kitakua ni programu-endeshaji yake kwani itakuwa inatumia Android. Kila kampuni la simu linakimbilia tumia android —labda sababu ni kwamba ndio programu-endeshaji inayoongozwa kutumiwa na watumiaji wa simu janja na pia sababu nyingine kuu ni wingi wa apps zinazopatikana katika Android— Pata picha blackberry ikiwa na programu-endeshaji hiyo
Kwa sasa kampuni ya BlackBerry, zamani Research in Motion (RIM) ambao ndio watengenezaji wa simu hizo za Blackbery wapo katika mikakati ya kuhakikisha simu yao ikiingia sokoni inauza sana tena ikiwezekana kushindana na makampuni makubwa kama vile Samsung katika soko la simu janja.
Katika mkutano wa Code/Mobile uliofanyika katika ufukwe wa Half Moon huko california, Mkurugenzi mkuu wa Blackberry Bw.John Chen amesema kuwa “kampuni inaweza ikaangalia na kutafakari upya uwepo wake katika soka la simu kama haitatengeneza faida mwakani” Hii haimaanishi kuwa kampuni hiyo itajitoa katika biashara kabisa bali inaweza kufikiria fanya kazi nyingine
Vile Vile mkurugenzi huyo alikiambia kituo kimoja cha habari kuwa ili Blackberry wawe na faida inabidi waweze kuuza simu milioni tano (5) kwa mwaka — Inawezekana sio?— Tumeshashuhudia makampuni mengi yakiuza zaidi ya hapo, ni malengo na vitendo tuu ndio yanayohitajika!
Inajulikana wazi kuwa watumiaji wengi wa simu za Blackberry ni wale wa kwenye makampuni makubwa na sekta nyeti za serikali wanaojilinda na usalama wa taarifa zao na hata serikalini bila kusahau raia wa kawaida. Simu mpya ikitoka yenye Android ndani yake itabadilisha kila kitu, watu wanapenda Android kutokana na wingi wa apps na hapo ndipo ninapopata imani kuwa itafanya vizuri kimauzo
No Comment! Be the first one.