Teknolojia inakua na mambo yanazidi kuwa mengi sana. Siku hizi watu wana akaunti nyingi za mitandao mbalimbali kiasi kwamba hadi wanaamua kutoingia katika mingine. Kwa mfano mtu anaweza akawa ana akaunti facebook, twitter, instagram, tango, badoo n.k na bado hapo sijataja akaunti za barua pepe.
Unapokuwa na akaunti nyingi kiasi hichi, kuifungua moja moja na kuanza kupitia ujumbe inaweza onekana kama kero. Na kuna watu wengine wanakua wapo bize sana na mda wao. Hebu fikiria kama meseji zote hizi ungezipata katika sehemu moja?
Kuna njia rahisi kabisa ya kusoma ujumbe kutoka katika mitandao kadha wa kadha kwa urahisi kabisa. Yaani haitakulazimu kufungua akaunti moja moja au kufungua app na kisha kuifunga ili ufungue nyingine. MOja kwa moja utasoma zote kwa kutumia App moja.
Digsby ni App ambayo inakuwezesha kusoma ujumbe kutoka katika mitandao mingi ya kijamii na pia hata katika barua pepe zako kwa kutumia App moja tuu.
Unachotakiwa ni kutengeneza akaunti na kisha kuingia katika akaunti unazotaka kusoma meseji kwa kutumia Digsby. Kisha kila utakapotumiwa ujumbe utaweza kuusoma ndani ya App hiyo.
Digsby mpaka sasa inaruhusu kuunganisha Gmail, Yahoo, Facebook, Twitter, LinkedIn, akaunti za barua pepe na nyingine kadhaa. Endapo mtu akikutumia ujumbe katika mitandao hii App ya Digsby itakujuza na kisha unaweza jibu ujumbe huo moja kwa moja ukiwa katika App hiyo.
Unaweza ukatuma meseji kutoka Digsby moja kwa moja. Na pia unaweza hata ukatuma ule ujumbe wa kiautomatiki, kwa mfano kama una kazi ya maana unafanya na usingependa mtu akusumbue/bugudhi unaweza ukatuma meseji moja kwa kila mtu. Unaweza Ukatuma ‘Niko bize, ntarudi kwako nikipata muda’ na ukaituma ikaenda kwa akaunti zote amabazo umeziunganisha na Digsby.
Angalia Video Fupi Ikijaribu Kuelezea App Hii
[iframe id=”https://www.youtube.com/embed/16grAzndW9w”]
Jinsi Ya Kushusha
Bofya Hapa ili kuipakua App hii katika kompyuta yako (windows). Bofya Download, na kisha App itaanza kushuka katika kompyuta. Ikikamilika i’click’ na uendelea fuata maelekezo yake. Ikishafunguka itakuomba ujiunge na App hiyo ya Digsby kwa kuomba Email yako.
Hii ni App nzuri sana kuwa nayo hasa kwa mtu mwenye mambo mengi (mtu bize) kwani inarahisisha mengi sana. Kwa mfano kwa watu wale walio maofisini na wanafanya kazi inakuwa na msaada mkubwa, baada ya wao kufungua na kufunga akaunti zao nyingi wanaweza wakatumia App hii moja kwa moja
Keep it up bro