fbpx

Gemu, Kompyuta, Laptop, Teknolojia

Acer waja na laptop 2 mpya: Nyembamba zaidi, na ya kwanza ya ‘display’ iliyopinda

laptop-za-acer-predator-21-x-swift-7

Sambaza

Acer watambulisha laptop 2 mpya zenye sifa za kipekee. Acer Swift 7 ni laptop nyembamba zaidi, wembamba wake hauzidi sentiminta moja (inchi 0.39), na Acer Predator 21 X ndio laptop ya kwanza kuja na kioo (display) chenye mpindo (curved).

Acer Swift 7

laptop ya acer swift
Muonekano wa Acer Swift 7

Laptop ya Acer Swift 7 ndiyo inachukua sifa ya kuwa laptop ya kwanza duniani kuwa na wembamba mdogo zaidi – ipo chini ya sentimita moja.

– Sifa zake

 • Inakuja na Windows 10
 • Inakuja na prosesa ya kisasa zaidi kutoka Intel – Intel 7th-generation Core i5
 • Wembamba mm 9.98
 • Ina sehemu mbili za USB-C 3, sehemu ya earphone (jack)
 • Betri yake inaweza dumu masaa 9
 • Kioo (display) – Inchi 13.3 Full HD IPS
 • RAM GB 8, Diski uhifadhi (storage) SSD 256
 • Uzito wa kg 1.1
SOMA PIA  Apple yapata pigo baada ya taarifa kuhusu bidhaa zake kuvuja

Pia mfumo wake mzima ndani yake ni wa bila feni, kuna teknolojia ya upoozaji ya Intel Kaby Lake chip ambao unasaidia kupooza mfumo mzima wa laptop hiyo bila uhitaji wa feni ya ndani. Jumba lake (housing) lote limetengenezwa kwa marighafi za alumini (aluminium)

Acer Predator 21 X

laptop ya Acer Predator 21 X
UZITO WA KILO 8!!!!! Laptop ya Acer Predator 21 X ikiwa imebebwa na mtu.

Ukiachana na laptop ya Acer Swift pia wametambulisha laptop kwa ajili ya wapenda kucheza magemu ya kompyuta, hii inakuja kwa jina la Acer Predator 21 X. Laptop hii inachukua sifa ya kuwa laptop ya kwanza duniani yenye kioo (display) yenye pindo, yaani ‘curved screen’.

acer predator 21X
Muonekano
 • Laptop ya Predator 21 X inakuja na display  ya inchi 21 (2,560 x 1,080 resolution)
 • Prosesa ya 7th Generation Intel Core ikija na kadi mbili za NVIDIA GeForce GTX 1080 GPUs
 • Uwezo wa kubeba hadi GB 64 za RAM
 • Acer Predator 21 X inauzito wa kilogramu 8!
 • Uwezo wa kubeba diski za SSD za hadi ujazo wa TB 4 (GB 4,000+)
 • Kwa ajili ya kuhakikisha joto halikai ndani ya laptop hii inakuja na feni 5 za kusaidia kupoza 
SOMA PIA  Roketi ya Space X yatumika kwa zaidi ya safari moja! #Anga

acer predator 21 x

 

 • Pia teknolojia ya sauti na spika ya SoundPound 4.2 inatumika, yaani laptop ina spika 4 pamoja na subwoofer 2 ndani yake. Pia ubora wa kiwango cha sauti ni wa juu kupitia teknolojia ya Dolby Audio

Inakuja na teknolojia ya  ‘Tobii eye-tracking hardware’ ambayo inawezesha kioo cha laptop (display) kuweza kusoma macho ya mchezaji gemu kuona anatazama wapi na hivyo kuondoa kazi ya kipanya (mouse) katika kumsaidia mchezaji kugeuka n.k wakati anachezesha mtu katika gemu.

SOMA PIA  Saa ya kisasa isiyochajia na kitu chochote bali na joto la mwili wa binadamu

Pia keyboard yake inakuja na uwezo mkubwa wa teknolojia ndani yake, utaweza badilishi kiwango cha mwanga na rangi kwa herufi moja moja ya kwenye keyboard. Na pia inaitaji nyaya mbili za umeme (2 power supplies) kuweza fanya kaziiiiiiii!!!

– Bei je?

Acer Swift 7 itaanza na bei ya Dola 1000 za Marekani (Tsh 2,180,000/= | Ksh 101,000/=) wakati bei ya Predator 21 X bado haijafahamika ila wengi wanaona itakuwa zaidi ya Dola 4000 za Marekani (Tunaongelea kwenye zaidi ya milioni 8 za Tanzania)!!!!!

Je unazionaje laptop hizi? Zaidi ya milioni 8 za Kitanzania kwa ajili ya laptop??

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |