fbpx

Uwekezaji wa Nokia kwenye afya na teknolojia ya VR

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Nokia ambayo kwa miaka mingi tu ilikuwa ikifahamika na kuwekeza kwenye teknolojia ya simu lakini sasa ipo kwa muda sasa kwenyesekta ya afya pamoja na “Virtual Reality”.

Nokia ilifanya vyema sana kwa miaka ya nyuma kutokana na simu zake kutokea kupendwa lakini kwa miaka ya hivi karibuni Nokia imekuwa ikifanya vibaya katika biashara na kufikia hatua ya Microsoft kuinunua kampuni ya Nokia karibu miaka mitatu iliyopita.

Withings-Kampuni iliyonunuliwa na nokia hivi karibuni

Withings-Kampuni iliyonunuliwa na Nokia.

Hata hivyo simu janja za Nokia zenye kutubmia Windows OS nazo zimekuwa hazifanyi vizuri katika soko la dunia kutokana kutovutia wateja wake na hivyo kufanya simu janja kutoka Samsung, Sony, Apple kupendwa zaidi na hivyo kuifanya Microsoft kupata hasara kutokana na simu janja zake kutopendwa.

Ozo camera yenye kutumia teknplojia ya virtual reality

Nokia waliamua kuja kivingine na kuja na teknolojia ya virtual reality na kutoa kamera iliyotokea kupendwa na watengeneza filamu kutoka mataifa mbalimbali. Hivi sasa kamera hiyo inauzwa $45 elfu.

Kutokana na kwamba Nokia wamenunua kampuni ijulikanayo kama “Withings” ambao wanatengeza vifaa vinavyotumika katika sekta ya afya ambavyo vipo kiteknolojia zaidi.

Vifaa vinavyotengenezwa na Withings ambayo ipo chini ya Nokia

Vifaa kwa ajili ya afya vinavyotengenezwa na Withings ambayo ipo chini ya Nokia.

Nokia wamesema kuwa wanatengeneza vifaa ambavyo si kwa ajili ya kufuatilia afya ya mtu bali hata mazingira ambayo yanamzunguka: Vifaa hivyo  vinafuatilia mazingira yanamzunguka mtu.

TeknoKona tutaendelea kukufahamisha mapya yoyote kuhusu teknolojia kutoka kona yoyote ya dunia. Maoni yako ni muhimu sana kwetu.

Vyanzo: Digital Trends, the verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Mfumo wa AI utakaoweza kufanya kazi bila intaneti unaundwa
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.