fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Maujanja Teknolojia

WinDirStat : Jinsi ya Kupata Nafasi KTK ‘Hard Disk’ Iliyojaa

WinDirStat : Jinsi ya Kupata Nafasi KTK ‘Hard Disk’ Iliyojaa

Spread the love

Umejaza filamu na nyimbo kibao katika diski yako, labda ni magemu pia. Tamthilia je? Inaweza ikawa moja ya vitu hivi au ni mambo mengine kibao yamejaa kwenye kompyuta yako kiasi ya kwamba inakuwa ni vigumu ata pa kujua mafaili makubwa ya kufuta ni yapi hasa.

Unaangalia kompyuta yako na inakuambia diski C yako inakaribia kujaa kabisa na hivyo unatakiwa ufute baadhi ya mafaili, ila ndio hivyo tena kutokana na jinsi yalivyomengi hufahamu mafaili yapi ni makubwa au yapo wapi hayo makubwa kutokana na wewe kuwa na mafolda mengi kwelikweli. Leo tunakutambulisha kwa programu moja ya bure kwa watumiaji wa kompyuta/laptop za Windows, inaitwa WinDirStat.

SOMA PIA  Huduma ya Dropbox yafikisha watumiaji zaidi ya Milioni 500

Ndio kuna njia zingine za kupunguza nafasi katika diski yako kama vile kutumia programu wa Windows ifahamikayo kama ‘Disk Cleaner’, ila hiyo haikuoneshi mafaili yako mwenyewe. Yenyewe inasaidia mafaili ya system ya kompyuta tuu.

Programu ya WinDirStat inakupa uwezo wa kufahamu mafaili gani ni makubwa na ni kwa ukubwa gani na pia inakupa uwezo wa kuyafuta kwenda kwenye ‘Recycle Bin’ au kuyafuta moja kwa moja kabisa bila kupitia Recycle Bin.

Pia kwa kutumia rangi mbalimbali utaoneshwa mafaili muhimu ambayo si vizuri uyaguse
Pia kwa kutumia rangi mbalimbali utaoneshwa mafaili muhimu ambayo si vizuri uyaguse
SOMA PIA  Vijana Watanzania waleta Soka ya Ligi Kuu Tanzania kwenye SImu!

Unaweza kushusha WinDirStat bure kabisa hapa -> http://www.fosshub.com/WinDirStat.html

Soma pia;

Diski ya 8TB Kutoka Seagate Yaingia Sokoni!

Samsung Wakuletea Diski ya TB 1 SSD Inayotosha Kiganjani

Je ungependa kuendelea kusoma habari zetu? Tutafurahi kama utaungana nasi kwenye akaunti zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania