Sikukuu ya wajinga ya mwezi aprili ndio hiyooo! na hii ni njia mojawapo ya watu wanaojihusisha na teknolojia kutengenaza michezo flani hivi kwa ajili ya siku hiyo.
Google hawajawahi kuangusha watu katika kipande hichi, hasa pale kampuni hiyo nguli (Google) inapoungana majeshi na magemu duniani
Mwaka huu Google Maps inawawezesha watumiaji wake kucheza PacMan katika mtandao huo. Gemu hili utalicheza popote duniani (ulipo). Cha kufanya chagua eneo lolote au mtaa wenye kona kona nyingi kisha bonyeza alama ya PacMan kuanza kucheza. Kutokana na eneo ulilochagua unaahidiwa kupewa mchezo mzuri wenye kona ambazo ni rahisi kugeuka
Katika miaka iliyopita Google walishawahi kushirikiana na makampuni mengine yanayojihusisha na magemu (kwa sikukuu ya wajinga) kama vile the Pokemon Company, Game Freak na Nintendo ili kugeuza Google Maps kuwa uwanja wa kucheza PacMan
Moja kati ya Mbwembwe za Goolgle ambazo ni maarufu na hazihusiani na sikukuu ya wajinga ya mwezi wa aprili ni Google Nose Beta, ni kipangele chake cha utafiti ambacho kilikua kinaweza kutambua harufu, kwa mfano kama ulitaka kujua pyramid za Egypt zinanukiaje, ungeweza jua. Google walifanya hivi ili watu wafikirie inawezekana kabisa kupitia Google Nose Beta
Kama Unataka kujua Zaidi Jinsi Google Nose Inavyofanya Kazi Angalia Video Hapa Chini
[youtube http://www.youtube.com/watch?v=VFbYadm_mrw&w=560&h=315]
No Comment! Be the first one.