fbpx

Facebook yabuni njia ya kuwavutia watu

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Facebook ambayo kwa kiasi fulani imepoteza uaminifu kwa wateja wake kutokana na mabo mbalimbali yaliyoikumba kampuni hiyo mwaka huu sasa wamebuni njia ya kuwavutia watu.

Kundi kubwa ambalo linatumia Facebook ni vijana na katika kujaribu kuwarudisha watu wahusika wametoa programu tumishi, TikTok (Lasso) ambayo kazi yake ni kuweza kusambaza picha jongefu fupifupi.

Programu hiyo inalenga vijana wanaochipukia ambao kwa ndio kundi kubwa linalotumia mitandao ya kijamii. Kimsingi Lasso inakupa uwanja mpana wa kuweza kuwashikisha wengine picha za mnato kutoka kwenye simu yako au za kutengeneza muda huohuo.

njia ya kuwavutia watu

Lasso-Programu tumishi mpya mahususi kwa ajili ya kusambaza picha jongefu zisizozidi urefu wa sekunde 15.

TikTok inapatikana kwenye Android/iOS ukiwa na uwezo wa kujiunga kupitia jina/barua pepe pamoja na nywila unayotumia kuingia kwenye akaunti ya Facebook/Instagram au ukajiunga upya tu mara baada ya kupakua Lasso.

Vyanzo: TechCrunch, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Apple kushitakiwa na kundi la watumiaji wa iPhone dhidi ya ukiritimba kwenye soko la Apps
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.