Umekutana na meseji WhatsApp inayokuambia ubofye linki flani kupata toleo la WhatsApp Gold? Kaa chonjo, ni jaribio la kuathiri simu yako.
Mara kwa mara meseji za namna hii huwa zinasambazwa na watu katika WhatsApp bila ata kuchunguza taarifa hizi, ni hatari!
Inasemekana ujumbe unaosambaa kwa sasa ukisema mtu akibofya kwenye linki hiyo atapata toleo jipya kabisa la WhatsApp linaloitwa WhatsApp Gold – lengo kuu ni watu kudownload kirusi kinachoshambulia simu yako na kutoma data zako kwa watengenezaji wa app hiyo.
Mambo ya kufahamu;
- WhatsApp hawatakupa taarifa zozote kuhusu huduma zao mpya kupitia ujumbe wa meseji unasambazwa na watu wengine
- Toleo lolote jipya la WhatsApp likitoka litakuwa linapatikana kupitia Google PlayStore – utaenda kwenye ukurasa wa WhatsApp katika Google Play na kuweza kusasisha (update).
- Epuka link yeyote inayosema ni ya whatsapp na huku si anuani hii – www.whatsapp.com
- Usisambaze taarifa ambazo hauna uhakika nazo ili kuepusha wengine kuathirika, mtu akikutumia kitu ambacho si cha kweli mwambie ili naye aache kusambaza kwa wengine.
Je wewe ushapokea ujumbe wa namna hii? Jifunze kuepuka kubofya link usizoziamini zinazokuambia udownload kitu.
Soma Pia – Makala yote kuhusu WhatsApp – TeknoKona/WhatsApp