Programu maarufu ya mawasiliano dunia, WhatsApp imepata pigo kubwa lingine baada ya mwanzilishi wake mwingine Bw. Jan Koum kuachana rasmi kufanya kazi katika programu hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya kampuni ya Facebook.
Awali WhatsApp ilikuwa inamilikiwa na marafiki wawili, Jan Koum na Brian Acton ambao ndio walioiprogramu kabla ya kuiuza Facebook kwa dola Bilioni 19. Licha ya kuiuza kwa Facebook bado waliendelea kufanya kazi kama waajiriwa.
Mwanzoni mwa mwaka huu muanzilishi mwingine wa WhatsApp Brian Acton alitangaza kujiondoa na miezi michache baadae amefuatia rafiki yake Jan Koum kutangaza nae kujiondoa.
Waanzilishi wa WhatsApp, Brian Acton na Jan Koum
Jan Koum kupitia ukurasa wake wa Facebook alitangaza kujiondoa WhatsApp kwa kusema ameamua kuwa pembeni baada ya safari ya muda mrefu na kuwashukuru wote alioshirikiana nao katika kufanya kazi ya kuiendesha WhatsApp hivyo sasa ni muda wa kufanya mambo mengine mbali na teknolojia.
Kuondoka kwa waanzilishi hao wa WhatsApp kunaelezwa ni kutokana na wamiliki wa sasa, Facebook kukiuka moja ya makubaliano waliyowekeana wakati walipowauzia ya programu hiyo.
Bw. Juan ni mtu ambae anafahamika kupenda vitu vya kifahari mbali na teknolojia na ameacha kufanya kazi na WhatsApp ili aende kuangalia kwa karibu mali zake yakiwemo magari ya kifahari.
Moja ya masharti ni kwamba WhatsApp haitawekwa matangazo na itakuwa na usiri zaidi kwa watumiaji wake pamoja na kuwachukuwa wafanyakazi wote wa WhatsApp.
Sababu nyingine ya kuondoka kwa waanzilishi hao ni Facebook kuuza data za watumiaji wake kwa makampuni mbalimabali na kuongeza kipengele cha kusambaza data za WhatsApp kwa Facebook ambacho kilipingwa na watumiaji wengi duniani.
Hata hivyo imeonekana WhatsApp inaelekea kutumika kuwekwa matangazo kitu ambacho waanzilishi hao hawakukitaka tangu awali. Bado mpaka sasa hakuna matangazo kwenye WhatsApp lakini kuna viashiria vingi kuwa jambo hilo lipo njiani kuja.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.