fbpx
apps, Intaneti, Mtandao wa Kijamii

Twitter yaongeza idadi ya herufi za majina za watumiaji wa Twitter #Masasisho

twitter-yaongeza-idadi-ya-herufi-za-majina-za-watumiaji-wa-twitter-masasisho
Sambaza

Unakumbuka idadi ya herufi ambazo Twitter ilikuwa ikiruhusu kwaenye jina la akaunti ya Twitter? Unaweza usiwe unakumbuka au hata kufahamu kutokana na ukweli usipingika kuwa si watu wengi wanatumia wamejiunga na mtandao wa kijamii wa Twitter.

Ni miezi michache tu Twitter ilitangaza uamuzi wake wa kuongeza idadi ya mameno kutoka jumla ya maneno 140 kwa tweet noja na kuwa mara mbili yake (maneno 280) kwa tweet moja. Na sasa inaonekana ni zamu ya kuongeza idadi ya herufi za jina linaloonekana kwenye profile ya mhusika.

Awali Twitter iliruhusu herufi za majina zisizozidi ishirini (20) kwenye jina la akaunti la mtumiaji wa Twitter na sasa imeamua kuongeza mpaka herufi 50.

Hii ina maana ya kwamba jina ulatumia kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter unaweza ukaongezea jina la katikati, ukoo, jina lako maarufu, n.k na kama ukitaka kuliremba zaidi unaweza ukaongezea na emoji ili mradi tu maneno yote kwenye jina hilo yasizidi herufi/alama maalum hamsini.

INAYOHUSIANA  Hizi ndio apps salama zaidi kwa kuchati - ripoti ya Amnesty International, 2016!
Akaunti ya TeknoKona Twitter: Mathalani tukiamua kuongeza jina na kuwa “TeknoKona Group Limited”. Tufuatilia kupitia twitter.com/teknokona.

Uwezo wa kuhariri jina la linaloonekana kwenye akaunti yako ya Twitter unaweza kufanya kupitia kwenye app ya Twitter au hata kupitia kwenye tovuti yao (Twitter) kwa kuingia kwenye profile yako kisha unaenda kwenye edit profile kubadilisha jina lako upendavyo.

Twitter haijaazia kwenye jina tu bali ilishaleta mambo kadhaa kuvutia mtandao huo wa kijamii. Umelipokeaje suala zima la Twtter kuamua kuongeza idadi ya herufi za jina la mhusika kwenye mtandao wa kujamii wa Twitter?

Vyanzo: Gadgets 360, BGR India, Marshable

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

  1. Twitter Lite yaanza kupatikana katika baaadhi ya nchi - TeknoKona Teknolojia Tanzania
    December 5, 2017 at 7:02 pm

    […] Twitter Lite ikiwa na lengo la kuvutia watu na kuongeza idadi ya watu wanaotumia Twitter sasa inapatikana kupitia Google Play Store katika zaidi ya nchi 24 na Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo. […]