fbpx
apps, instagram, Maujanja, Mtandao wa Kijamii, Snapchat, Teknolojia

Rekodi Video Snapchat/Instagram Bila Kugusa Sehemu Ya Kurekodia Wala Mishale Ya Sauti (iPhone)! #Maujanja

rekodi-video-snapchatinstagram-bila-kugusa-sehemu-ya-kurekodia-wala-mishale-ya-sauti-iphone-maujanja

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Hivi ni mara ngapi ulisharekodi video zile za Instagram/Snapchat lakini vidole vikakuharibia (mfano, ukaifuta kwa bahati mbaya)? Licha ya hivyo tuu kuna muda mwigine tunashindwa kushika simu zetu vizuri na kupata ‘angle’ nzuri ya kurekodi video hizo.

Sasa kama wewe ni mtumiaji wa iPhone utakuwa na uwezo wa kufanya video hizo zijirekodi zenyewe wakati wewe ukiwa umetegesha simu tuu. Baada ya hapo utaweza kuzituma picha/video hizo katika mitandao yako ya kijamii (Instagram/Snapchat).

INAYOHUSIANA  Alibaba watambulisha Gari janja lililounganishwa na intaneti na OS

Fuata Haya.

1. Fungua sehemu ya Settings na kisha chagua General na kisha Accessibility.


2. Chagua Assistive Touch kwenye sehemu ya Interaction na kisha iwashe.

3. Bonyeza na kisha chezesha kidole (huku umeshikilia kioo) ili kutengeneza umbo la duara.

4. Baada ya hapo unaweza uka’save’ na ukaandika jina (video) lolote unalotaka.


5. Baada ya hapo utakuwa umeshaweza hatua ya kwanza. Sasa kilichobakia ni wewe kwenda katika mtandao wa Instagram/Snapchat.

INAYOHUSIANA  App ya Wiki: ES Explorer kwa Kushughulikia Mambo Mengi kwenye Android

– Ukishafunguka uwanja wa kupiga picha/video, bonyeza kile kiduara cha Assistive Touch alafu nenda katika Custom na kisha Video (au jina lolote ulilolihifadhi mwanzo)


6. Baada ya hapo utakiona kiduara kingine kidogo kimejotokeza, hapo unatakiwa kukishikilia na kukisogeza katika duara kubwa la kupigia picha la Instagram/Snapchat na kisha utashuhudia maajabu ya teknolojia.


Mpaka hapo na wewe umeshakuwa mtaalamu sio? Kumbuka utakuwa huna haja tena ya kuanza kubonyeza kile kiduara katika Snapchat/Instagram Ili kuredi video. Hapa utakuwa kama bosi hivi, utashika tuu simu huku yenyewe ikifanya yake.

INAYOHUSIANA  Huawei kutoa mafunzo kwa wahitimu wa vyuo

Niambie hii umeipokeaje? Niandikie hapo chini sehemu ya comment. Ningependa kusikia kutoka kwako. TeknoKona daima tupo nawe katika teknolojia!.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com