fbpx
Facebook, instagram, Mtandao wa Kijamii, Snapchat, Teknolojia, Uchambuzi

Muda mchache kwenye mitandao unapunguza upweke

muda-mchache-mitandaoni-kuondoa-upweke
Sambaza

Watu wengi duniani wanatumia sehemu ya muda wao kutembelea mitandao ya kijamii jambo ambalo limebainika kuwa na madhara hasa kiafya lakini iwapo utatumia muda mchache kuperuzi basi utakuwa umepunguza msongo wa mawazo/upweke.

Zipo tafiti mbalimbali ambazo zimeshawahi kufanyika na kubainisha madhara ambayo yanatokana na kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii hasa kwa wale ambao wanafikia hatua ya kuripoti kwenye kampuni husika iwapo kuna kitu kimemkwaza kilichochapishwa kwenye mtandao wa kijamii husika.

Katika utafiti ambao ulijumusha wanafunzi mia moja arobaini na watatu (143) waliotakiwa kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii muda usiozidi dakika 10 kwa siku moja au kutumia kama ilivyokuwa kawaida yao. Utafiti huo ulidumu kwa muda wa wiki tatu na kila wiki walikuwa wanafuatiliwa maendeelo yao.

Matokeo ya utafiti huo yalibainisha wale walioweza kutumia mitandao ya kijamii kwa muda waliokuwa wameambiwa walionekana kupungua msongo wa mawazo na upweke.

Muda mchache
Kundi jingine lilweza kupunguza msongo wa mawazo/upweke ingaw si kwa kiasi kikubwa lakini wote wakiwa wameweza kupunguza hofu ya kukosa kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii.

Kiujumla utafiti huo haujaweka muda kamili ingawa wakapendekeza kutumia muda mchache (dakika 30) kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii utasaidia sana kukupunguzia upweke/msongo wa mawazo.

Vyanzo: TechCrunch, Science Daily

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Miaka 10 ya MacBook Air: Urithi wa Jobs kwa ulimwengu wa teknolojia
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|