fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android Apple apps iOS Teknolojia

App Ya ‘Move To iOs’ Gumzo Kwa Watumiaji Wa Android!

App Ya ‘Move To iOs’ Gumzo Kwa Watumiaji Wa Android!

Spread the love

Apple inarahisisha kuhamisha vitu vya muhimu kutoka katika simu yako ya Android kwenda katika ile ya iOs. Hebu fikiria, umejipatia simu mpya ya iPhone na una baadhi ya taarifa zako za muhimu katika simu yako ya Android ambazo inabidi uziweke katika simu hiyo mpya (iPhone).

Hutatoa jasho tena kama zamani, sasa kila kitu Apple wanakurahisishia. Ukitumia App hii meseji, picha, video, Taarifa za kivinjari (Bookmarks), akaunti za barua pepe, kalenda pamoja na  wallpaper vyote vitahamia katika kifaaa cha iOs (iPhone na iPad). Na Cha kuongezea ni kwamba kama kuna App yeyote ya kulipia katika simu ya Android zoezi hili likifanyika App hizo zitawekwa katika kundi la ‘Wish List’ katika kifaa cha iOs (iPad na iPhone)

App Ya ‘Move To iOs’ Katika Simu Ya Samsung

Zoezi Hili litakamilika kama kifaa chako cha iOs ni kipya au umeki ‘Reset’ tuu. Hii inamaanisha kwa vifaa vya iOs vile vilivyotumika kwa mfano kama umetumia iPhone yako na kisha ukasema unataka uhamishe taarifa zako kutoka simu ya Android itashidikana (Labda ui ‘Reset’ Hiyo iPhone Kwanza)

Tuangalie Habari Picha Jinsi Ya Kufanya Zoezi Hili

 1. Kwanza kabisa shusha App Ya ‘Move To iOs‘ katika simu yako ya Android.

  Katika Android Ingiza Kodi Uliyoipata Katika Kifaa Cha iOs Katika Sehemu Ya Kuanzia kwenye Kipengele Cha ‘Move Data From Android’

 2. Move-Data-from-Android-800x547

  Katika iPhone Bofya ‘Move Data From Android’ Ili Kupata Kodi Ya Kuingiza Katika Android ( Picha ya kwanza)

 3. Download-the-Move-to-iOS-app-785x600

  Katika iPhone, Maelezo Utayoyapa Kabla Ya Kuanza Kuhamisha Vitu Na Pia Simu Ikikushauri Kushusha App Ya ‘Move To iOs’ Katika Simu Ya Adroid Ili Kuanza Mchakato

 4. Enter-This-Code-800x576

  Katika iPhone Kodi Utakayoiona Iingize katika Kifaa Cha Android (Kama Picha Ya Kwanza Inavyodai)

 5. Baada Ya Hapo Simu Mbili Zitaungana Na Hatimaye Kuanza Kuhamisha Vitu Kutoka Android Kwenda iOs

 6. Uhamisho Utaanza Kwa 0% Mpaka 100% (Ukamilike)

 7. Transfer-Complete-772x600

  Katika iPhone Ikionyesha Uhamisho Umekamilika

Zoezi zima la kufanya yote haya ni rahisi na kila mtu nna imani anaweza fanya mwenyewe. Japokuwa App hii katika Google Play store imepata mapokezi hasi (si mazuri) kwa watu wengi na wengi wao wakiwa ni watumiaji wa Andriod. Licha ya mapokezi hayo App hii bado ina msaada mkubwa kwa wale wanaotaka kubadilisha mazingiza (kutoa Android mpaka iOs)

Baadhi Ya Watumiaji Wa Android Wakionyesha Kutoridhishwa Kwao Na App Hii

Move to iOS [Android]

Kutokana na yote hayo, kuna mengi ya kujiuliza kama hili, Je Apple watakua tayari kurudisha uungwana huu walio upata kutoka kampuni la Google (ALPHABET) wakitaka kuleta App kama hii ila kwa watumiaji wa Android “Move To Android”?. Maana mpaka sasa App hii haijafutwa katika Google Play Store. Nipe mawazo yako juu ya hili. Ningependa kusikia kutoka kwako. Kwa nyingine kama hizi tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKonaDotCom. TeknoKona Tupo Nawe Katika Teknolojia

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania