Mtandao wa Facebook unafanya kila kinachowezekana kuhakikisha kinawaweka wateja wake wakiwa hewani muda wote wa siku kwa kuanzisha huduma za habari, video, kuchati na vingine. Sasa, imezindua mfumo mpya kabisa, ambao hata ivyo ni mwendelezo wa kile ulichokua tayari kukifanya kila siku, kushinda mtandaoni siku nzima ukiwa Facebook.
Kampuni fulani sasa inaweza ikaandaa mtandao wao wa kijamii, utakaowaunganisha wafanyakazi wote, na kufanya mambo yanayohusiana na kazi tu.
Wakiuita Facebook Kazini (Facebook At Work), mfumo huu ulizinduliwa mapema wiki hii, ambao utakua unafanya kazi kama Facebook ya kawaida, japo sasa utaungana na wenzako ambao wanaweza kuwa au wasiwe Marafiki zako. Cha muhimu zaidi ni kwamba, sasa Bosi wako kazini hatakukoromea akikukuta ukiwa Facebook, kwani ata kama utakuwa Facebook, bado utakuwa unafanya kazi.
Kwa sasa, Facebook wamethibitisha kuachia mfumo huo kwa baadhi ya washirika wake wa karibu kwa majaribio maalum, wakiwa na matumaini ya kuachia kabisa mapema siku za usoni. Tayari App za IOS zimeshapakiwa kwa ajili ya majaribio ya jumla. Wenyewe wanasema wamekuwa wakitumia mfumo huu ndani ya ofisi zao kwa miaka mingi tayari.
“Wakati bosi wetu (Mark Zuckerberg) alipotutangazia, alitumia Facebook Kazini kutujulisha kuwa dunia itaanza kutumia mfumo huu mpya.” Anasema Lars Rasmussen, Mkurugenzi mkuu wa Ukandarasi wa Facebook
“Tumegundua kuwa, kutumia Facebook kama sehemu ya kazi kunafanya siku zetu za kazi kuwa bora zaidi. Unaweza kukamilishwa mipango mingi zaidi ya kazi ukitumia Facebook, kuandaa mikutano, kukutana na Washirika, kuanzisha lengo la kwapamoja miongoni mwa watu wenye lengo moja.” Anafafanua Lars.
“Kufanya kazi kwa makini” na “kushinda ukiwa Facebook kazini” ni masuala yanayokinzana kabisa kwani kufanya kazi mbovu mara nyingi kumehusishwa na kuwa mvivu na kuwa kwenye mitandao ya kijamii kwa wafanyakazi wengi. Lakini kama kushinda Facebook kunaweza kukailetea kampuni Faida kubwa, Hakuna namna matajiri wanaweza kukuzuia kufanya ivyo.
JINSI INAVYOFANYA KAZI
Kwa namna ambavyo Rasmussen alivyoelekeza, Facebook kazini itakua na mwonekano wa kawaida kabisa, kurasa zinazofanana na kurasa tulizozizoea, app na vifaa tunavyotumia kawaida. Itakuwa inatumika kama sehemu ya kompyuta ya mezani, au kama app kutoka Android na App za IOS.
Tofauti kubwa itakuwa kwenye mfumo wa rangi utakaotumika, ambao nembo ya facebook itakuwa na rangi tofauti itakayokuwa rahisi kutofautisha na Facebook ya kawaida hivyo kuwa rahisi kuelezea kama unatumia Facebook kwa matumizi binafsi au Facebook Kazini.
Mtakapoungana Washirika, mfano wafanyabiashara, wakandarasi tu, walimu, watoa bima, au madereva n.k. mtakuwa na kurasa zenu wenyewe, messenger zenu wenyewe, mfumo wa kuongea kupitia video utakaowakutanisha kirahisi zaidi. Hutakuwa na haja ya kuwa na akaunti binafsi kutumia Facebook kazini. Kama kampuni itajisajili, basi wafanyakazi wake wataweza kutumia kwa matumizi ya kampuni.
Unaujua mtandao wa LinkedIn? Facebook At Work utafanya kazi kama vile, japo kuna vingi vipya zaidi vimeongezwa, na vingine vinavyolandana sana na huduma nyingine kama zile za Microsoft za Yammer, Slack, Convo, Socialcast na nyingine ili kukutanisha wafanyakazi wa aina moja.
Sasa kurasa zako za Facebook zitatawaliwa na habari zinazotumwa na wafanyakazi wenzako, au watu wanaofanya kazi kama zako. Habari hiyo itaendelea kusambaa mpaka itakapoonekana na kampuni nzima.
Facebook wanatazamiwa kufanya huduma hii kuwa bure, kwani lengo kuu lao ni kupata watumiaji wengi zaidi watakaokuwa hewani. Sasa Facebook Kazini itafanya watumiaji kushindwa kukosa kuwa hewani.
Chanzo cha Makala haya ni mitandao ya W.I.R.E,D, GCAI, na mtandao wa TC
No Comment! Be the first one.