Makamu wa Rais mkuu wa kampuni ya kuuza chakula Walmart amesema katika ukurasa wao wa habari kuwa kwa sasa wateja wa kampuni hiyo wataweza kuagiza vyakula kupitia vifaa vyao vya mawasiliano vya nyumbani pia katika simu zao kwa kutumia kifaa cha kiroboti cha sauti cha Google.

Uwezo huo wa kutumia kifaa cha sauti cha google (Google Assistant) kuagiza kifaa utaunganishwa kwa kila akaunti kuanzia wiki hii hivyo watumiaji wa walmart wategemee kupata huduma hii mpya kutoka kwa kampuni yao pendwa.
Je kama wewe ni mteja wa kampuni ya Walmart unaonaje njia hii mpya ya kuagiza vyakula?